BM BARBERSHOP KINONDONI

Monday, September 10, 2012

BARABARA YA SEGERA MKUMBARA SAME YAANZA KUJENGWA BAADA YA MIKATABA MIWILI KUSAINIWA

Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale amewekeana Saini Mkataba wa Ujenzi wa Barabara ya Segera Mkumbara Same yenye urefu wa Kilometa 172 itakayogharimu jumla ya shilingi shilingi 62,866,110,284 za Kitanzania. Mkataba huo umegawanywa mara mbili na kukabidhiwa kwa kampuni mbili za Strabag International ya Ujerumani itakayo kabati eneo la Segera-Korogwe- Mkumbara kwa Urefu wa km76 na Kampuni ya DOTT Services Ltd kutoka Uganda itaanzia  Mkumbara – Same kwa urefu wa Km 65.

Hafla hiyo pia imeshudiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt, John Magufuli, Makamu Mwenyekiti Kamati ya Miundombinu ambae pia na Mbunge wa Same Mashariki Anne Kilango Malecela, pamoja na watendaji wa ngazi za juu wa Wizara ya Ujenzi na wadau wa sekta hiyo.

Baadhi wa wakandarasi kutoka kampuni ya ya Strabag International Gmbh ya Ujerumani wakisubiri kuweka saini mkataba wa ukarabati wa barabara ya kutoka Korogwe- Mkumbara- Same katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya ofisi za Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS ) jijini Dar es Salaam Jan,26.2012. (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) akiwekeana saini mkataba wa ukarabatiwa barabara ya Korogwe- Mkumbara- Same pamoja na Mkandarasi kutoka kampuni ya Strabag International GmbH ya Ujerumani Meneja Biashara kwa Afrika Mashariki Bw Karl Henz Schneder, (kulia) jijini Dar es Salaam, Hafla hiyo pia imeshudiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt, John Magufuli (katikati alievaa miwani) akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti Kamati ya Miundombinu ambae pia na Mbunge wa Same Mashariki Anne Kilango Malecela, pamoja na watendaji wa ngazi za juu wa Wizara ya Ujenzi na wadau wa sekta hiyo,Ukarabati huo wa km 172 utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 12 za kitanzania, ambapo kampuni hii itakarabati kipande kutoka Korogwe- Mkumbara (76 km) na kugharimu zipatazo shilingi bilioni 63
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) akitoa taarifa ya mradi wa ukarabati wa barabara ya Korogwe- Mkumbara- Same (km 172) jijini Dar es salaam katika hafla ya uwekaji saini Jan,26,2012, (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) pamoja na Mkandarasi kutoka ya DOTT Services Ltd kutoka Uganda ambae ni Meneja Mkuu Bw.G,Prudhvi Raj wakibadilishana Nyaraka baada ya kusaini mkataba wa ukarabati wa ujenzi wa barabara ya Korogwe- Mkumbara- Same

Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) akibadilishana hati na - Meneja Biashara kwa Afika Mashariki Bw, Karl Henz Schneder wa kampuni ya STRABAG International GmbH ya Ujerumani baada ya kusaini mkataba wa ukarabati wa barabara ya Korogwe- Mkumbara- Same

No comments:

Post a Comment