Na. Mbaruku Yusuph, Tanga
BARAZA
Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Mkoa wa Tanga limemuunga mkono Sheikh Mkuu
wa Tanzania, Mufti Issa bin Shaban Simba kwa kumteua Sheikh Abdallah Mnyasi
kuwa Kadhi Mkuu wa Tanzania.
Akizungumza
na Tanzania Daima jana, Sheikh wa Mkoa wa Tanga, Ally Juma Luwuchu, alisema
uamuzi wa Mufti Simba ulikuwa sahihi, halali na ulizingatia maslahi ya Waislamu
wote. Alisema uteuzi wa Sheikh Mnyasi ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la
Ulamaa Bakwata ulitokana na kikao halali cha Tume ya Dini cha masheikh wote wa
mikoa na wilaya zake kilichofanyika Juni mwaka huu, mjini Dodoma.
Sheikh
Luwuchu alisema Bakwata imekwishatayarisha mfumo wa kisheria utakaokidhi
mahitaji ya Waislamu katika kushughulikia kesi za mirathi, ndoa na waqfu. Alisema
jukumu lililopo kwa masheikh wote wa mikoa na wilaya zote hapa nchini ni kuunga
mkono juhudi zinazofanywa na Mufti Simba kuitisha kikao cha Tume ya Dini na
wakati umefka sasa kwa Waislamu kuungana katika kuleta maendeleo ya Uislamu
nchini.
Chanzo: Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment