![]() |
DAUDI MWANGOSI WAKATI WA UHAI WAKE |
DAUD
MWANGOSI KULIA ENZI ZA UHAI DAKIKA 20 KABLA YA KUUWAWA KWAKE
|
MWILI WA DAUDI MWANGOSI UKIWA UMEHARIBIKA VIBAYA |
Aidha taarifa kupitia Blog Mbalimbali zimeeleza kama ifuatavyo:
Mwandishi wa habari wa Channel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chama chama
cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za
Polisi na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani
Iringa leo. Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni
katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa
risasi.
Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa hawapo tayari kuondoka katika ofisi yao. Chanzo cha mwanahabari huyu kufariki kilitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa, Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kutaka kuhoji Polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo, ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini.
Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa 'afande nimekufa' ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti. Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya. Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wakijeruhiwa.
JESHI la Polisi Mkoa wa Iringa limesema limezuia
mikutano ya vyama vya siasa kwa vyama vyote na sio kwa chama cha Demokrasia na
maendeleo (CHADEMA) pekee hivyo inaonya vyama vyote kutii sheria bila shuruti. Hata
hivyo jeshi hilo la Polisi limesema kuwa halifanyi kazi kwa matakwa ya chama
chochote cha siasa na kuwa si kweli kama wanavyodai viongozi wa Chadema kuwa
jeshi la polisi linatumiwa na chama cha mapinduzi (CCM) kuzuia mikutano hiyo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael
Kamuanda ametoa kauli hiyo leo ofisini kwake alipozungumza na waandishi wa
habari kuhusu zuio la Mkutano wa Chadema uliopangwa kuanza leo katika Wilaya ya
Mufindi.
“Nawatangazia wanasiasa na vyama vyote vya siasa
pamoja na wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa hakutakuwa na mikutano ya kisiasa
kutokana na shughuli za sensa zinazoendelea ....hivyo basi nawaomba wananchi
wote kutoshiriki mikutano yoyote ya kisiasa itakayoitishwa na wanasiasa "alisisitiza
Kuwa mikutano hiyo imezuiliwa kwa kipindi hiki cha
sensa kilichoongezwa hadi hapo tamko litakapotolewa tena na msajili wa vyama
vya siasa John Tendwa kama alivyokwisha kutoa tamko la kuzuia shughuli hizo za
vyama vya siasa kwa kipindi hiki cha sensa.
"Wananchi wote wa mkoa wa Iringa mnaombwa
kutii sheria bila shuruti hii ni amri ....nawaombeni sana wananchi
kutodanganywa na wanasiasa kwa kuvunja sheria "aliongeza kamanda huyo wa
polisi.
Hata hivyo alisema kuwa kimsingi zoezi la sensa
lilipaswa kuhitimishwa Septemba mosi mwaka huu ila kutokana na serikali
kuongeza muda wa zoezi hilo bado jeshi hilo la polisi linazingatia maagizo ya
Msajili wa vyama vya siasa kama alivyoyatoa kwa jeshi hilo.
Kamanda Kamuanda alisema kuwa jeshi hilo la polisi
wala msajili wa vyama vya siasa hajazuia vyama vya siasa kuendelea na vikao
vyao vya ndani kwa kipindi hiki na kuwa hata Chadema wakiwa mkoani Iringa
wameendelea kufanya vikao vyao vya ndani katika kata mbali mbali za mkoa wa
Iringa na hakuna mtu aliyewazuia kuendelea kufanya hivyo.
MAJIBU YA KATIBU
WA CHADEMA DR. WILBROAD SLAA
Wakati jeshi la polisi likipinga shughuli hizo za
vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara katibu mkuu wa Chadema Taifa Dkt
Willbroad Slaa ameibuka na kusema kuwa chama chake kitaendelea na mikutano kama
kilivyojipangia na kuwa wapo tayari kwa lolote litakalojitokeza .
Dkt Slaa alisema kuwa walivumilia mara ya kwanza
walipozuiwa mikutano hiyo mkoani Iringa na kuvuta subira hadi jumamosi zoezi
hilo lilipomalizika sasa anashangazwa kuona jeshi hilo likiendelea kuzuia
mikutano hiyo tena.
"Tumemsikiliza kamishina wa sensa Hajati Amina
Mrisho Said kuwa hadi sasa watu asilimia 95 wameandikishwa huku akiwata wale
ambao bado kuwapigia simu wenyeviti wa mitaaa na vijiji ili wakaandikishwe na
makarani wa sensa ....sasa jeshi la polisi linataka kutuambia kuwa hao watu
asilimia 5 waliobaki wapo Iringa peke yake hadi wakazuia mikutano yetu?
tunasema hatutakubali tutaendelea na mikutano yetu kama kawaida hatupotayari
kabisa kusubiri hadi tarehe nane" alisema Dkt Slaa.
No comments:
Post a Comment