
Coast ndio waliokuwa wa kwanza
kuandika bao mapema kipindi cha kwanza likifungwa na kiungo wake Razak Khalfani
kwa shuti kali la mbali lililomshinda mlinda mlango wa Yanga Ally
Mustafa'Bartez'.
Mabao ya Yanga yalipatikana katika
kipindi cha pili, la kwanza likitokana na mpira wa kujifunga baada ya krosi
kali ya Shamte Ally na mchezaji Philipo kuusindikiza mpira Wavuni kwa kichwa. Bao
la pili lilifungwa na Said Bahanuzi “Spider Man” kwa shuti kali lililogonga mwamba na kisha kutinga wavuni.
Coast walilazimika kucheza pungufu katika
sehemu kubwa ya kipindi cha pili cha mchezo kufuatia kiungo wake Jeri
Santo kutolewa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu baada ya kutoa lugha chafu kwa
mwamuzi.
Aidha katika mchezo wa jana nusura
ulsichezwe baada ya kutokea hali ya sintofahamu muda mfupi kabla ya mchezo
kuanza. Sintofahamu hiyo ilisababishwa na uchelewaji wa timu ya Coastal Union
ambayo iliingia uwanjani saa 10:14 na kuanza kupasha viungo wakati muda wa
kufanya hivyo ulikuwa umesha kwisha. Mchezaji wa zamani wa Coastal Union Juma
Mgunda ambaye ndiye Kocha wa timu hiyo pamoja na Habibu Kondo waliendelea
kuwapa mazoezi wachezaji wao wakati refa alipowataka kuingia Vyumbani kwa
ukaguzi.
Refa wa Mchezo huo aliwaita Yanga na
kuingia nao uwanjani na kufanya ukaguzi kwa mujibu wa Sheria inavyotaka.
Coastal waliendelea kukaidi agizo la Refa hivyo Kocha wa Yanga aliamua kuitoa
timu Uwanjani na kuelekea vyumbani. Hekima ilitumika kuwashawishi Yanga kurejea
uwanjani na hatimaye mpira ukachezwa.
No comments:
Post a Comment