CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesitisha mikutano yake ya Oparesheni
Sangara na Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), iliyokuwa ikiendelea mkoani Iringa.
Alisema
uamuzi huo umefikiwa na viongozi waliokuwa wakiratibu operesheni hiyo ili
waweze kurudi Dar es Salaam ambapo Jumapili wiki hii watakutana na Kamati ya
Halmashauri Kuu kujadili vurugu hizo ambazo zilitokea wilayani Mufindi.
“Tumeamua
kusitisha operesheni zetu kwa muda ili tukakakutane na Kamati ya Halmashauri
Kuu tuweze kujadili matukio yaliyojiri likiwamo la kuuawa kwa mwandishi,”
alisema Bw. Yusuph.
Katika
hatua nyingine, Bw. Yusuph amemtupia lawama Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Mkoa
hapa, Charles Kamuhanda na kudai ndiye chanzo cha vurugu zilizotokea Kijiji cha
Nyololo.
Alisema
baada ya viongozi wa CHADEMA kuwasili na Kamanda wa operesheni hiyo, Bw. Single
Kigairo, katika eneo la Nyololo, polisi waliwazuia kufanya mikutano ya hadhara.
“Sisi
tulikubaliana na agizo lao lakini tulimuomba Kamanda wa Polisi Wilaya ya
Mufindi ili tufungue matawi ya chama na alikubali pamoja na kuwapa maelekezo
askari wake wasifanye lolote, baada ya makubaliano hayo tulifanikiwa kufungua
tawi la kwanza.
“Wakati
tukiwa katika harakati za ufunguzi wa tawi la pili, ghafla aliwasili Kamanda
Kamuhanda na kuamuru wafuasi watu wakae chini na kunyoosha mkono juu mikono juu
agizo ambalo tulilizingatia bila matatizo,” alisema.
Aliongeza
kuwa, jambo la kushangaza Kamanda Kamuhanda aliagiza wafuasi wa chama hicho
wakamatwe ndipo vurugu hizo zilipoanza kutokea na kusababisha mauaji.
Akizungumzia
mazingira yaliyosababisha kifo cha Mwangosi, alisema Polisi ndio waliomuua
wakati akimtetea mwandishi wa Gazeti la Nipashe, Bw. Godfrey Mushi, ambaye
alikamatwa na Polisi na kushambuliwa wakati akikimbia moshi wa mabomu.
Alisema
kabla ya kukumbwa na umauti, marehemu Mwangosi alikuwa akirekodi matukio ya
siku hiyo lakini baada ya vurugu hizo kuanza, kila mmoja alianza kutafuta njia
ya kuokoa maisha yake
CHANZO MAJIRA
No comments:
Post a Comment