MCHEZAJI raia wa Brazil, Adriano, amewaacha
midomo wazi viongozi wa timu yake mpya ya Flamingo baada ya kushindwa
kuhudhuria mazoezi ya klabu hiyo na kukutwa kwenye baa ya uswahilini akikata
kilaji ikiwa ni siku 13 tangu ajiunge na timu hiyo. Adriano aliyeichezea timu
ya taifa ya Brazil mechi 48 na kufunga mabao 27, alipigwa picha akiwa kifua
wazi kwenye baa ya uchochoroni kwenye mazingira machafu huko Vila Cruzeiro huku
wachezaji wenzake wakiendelea na mazoezi.
Mshangao mkubwa unatokana na ukweli kwamba,
mchezaji huyo wa zamani wa Inter Milan ya Italia, alieleza kuwa kutua kwake
Flamingo ni nafasi yake ya mwisho kurekebisha tabia zake za nje ya uwanja na
kuonesha kiwango kizuri ili arudi kwenye kikosi cha taifa na kukiwakilisha
kwenye michuano IJAYO.
No comments:
Post a Comment