BM BARBERSHOP KINONDONI

Tuesday, September 4, 2012

DAUDI MWANGOSI AZIKWA PATA TUKIO ZIMA KWA PICHA


PICHA ZOTE NI KWA HISANI YA MBEYA YETU BLOG
Mpiga picha Mkuu alikuwa ni Ndugu Joseph Mwaisango  na
Waandishi wa Habari na Wanakijiji wakiwa wamebeba Mwili wa Marehemu Daudi Mwangosi kuelekea Makabirini
Ibada ya Mwisho ya Marehemu Daudi Mwangosi kabla ya kuingizwa Kaburini
Mwili wa marehemu Daudi Mwangosi ukishushwa kwenye nyumba yake ya milele
Mwili wa Marehemu Daudi Mwangosi ukiwa ndani ya Kaburi
Mazishi yanaendelea 
Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi akiweka Shada la Mauwa kwenye Kaburi la Mume wake kwa machungu
Mke wa Daudi Mwangosi alishindwa kujizuia hapa akiwa amelala kwenye Kaburi la Mumewe akiwa analia kwa uchungu mwingi inasikitisha sana
Ni ngumu sana Kuamini kwa mke wa Marehemu lakini hali ndivyo ilivyo kuwa akiwa na huzuni kubwa
Watoto wa Marehemu wakiwa wanaweka mashada ya maua kwenye Kaburi la Baba yao hawatamuona tena 
Waandishi wa Habari walikuwa makini kuhakikisha wanapata Picha kwenye kila hatua wakati wa Mazishi
Mbunge wa Jimbo la Rungwe na Waziri asiye na Wizara Maalum Mh. Prof. Mark Mwandosya akiweka Taji la maua pamoja na mkewe
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr Willboard Slaa akiweka Shada la Mauwa  kwenye Kaburi la Marehemu
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr Willbroard Slaa ameshaweka shada
Rais wa UTPC akiweka shada la Maua
Mwandishi Mkuu wa Mbeya  yetu, Ndugu Joseph Mwaisango akiwa anatoa heshima zake za Mwisho katiaka Kaburi
Ndugu wa Marehemu akiweka shada la Maua
Mwenyekiti wa Mbeya Press Club akiweka shada la maua 

Hivi ndivyo jinsi safari ya Mwisho Ndugu yetu, Mwanaharakati, Mpiganaji Daudi Mwangosi aliyekuwa Mwandishi wa Chanel 10.

TONE MULTIMEDIA COMPANY LIMITED AMBAO NI WAMILIKI WA MTANDAO WA MBEYA YETU, WANAWAPA POLE SANA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WALIOPATWA NA MSIBA MKUBWA, KAMA WANAHABARI PIA WAMESIKITIKA SANA KUTOKANA NA MSIBA HUU. MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU.

No comments:

Post a Comment