BM BARBERSHOP KINONDONI

Wednesday, September 5, 2012

KIKAO CHA TAWI LA YANGA FACEBOOK CHARUDISHWA NYUMA SIKU MOJA


Kikao cha Kawaida kinachokusudia kuwakutanisha Wadau wa Timu ya Yanga ndani ya Facebook kimerudishwa nyuma siku moja tofauti na ilivyokuwa imepangwa. Akiongea na Mwanatanga wakati anawasilisha mabadiliko haya Mwenyekiti wa Tawi hilo Ndugu Innocent Mwingira amesema kuwa sababu za Mabadiliko hayo ni kutokana na uwezekano wa Mechi ya Simba na Azam kuangukia siku ya Jumapili tarehe 09/09/2012 ambayo ndiyo ilikuwa imepangwa hapo awali. Pia Mwenyekiti amehanikiza kuwa wamejaribu kuangalia eneo ambalo litakuwa ni rahisi kufikika kwa kila mjumbe ambalo sasa wamependekeza kuwa Afri Center Ilala Boma. Taratibu za Ukumbi pamoja na mambo mengine kuhusiana na Kikao hicho yanaendelea Vizuri. 

Mwenyekiti pia amewaomba Wadau ambao ndani ya Facebook wanakaribia 174 kuwa na utaratibu wa kujibu na kuchangia Hoja pindi zinapotolewa ili kupeana habari kwa Faida ya Yanga yao. Inasikitisha kuona mada inatolewa na uchangiaji unakuwa siwakutia moyo. Mfano mzuri ni mada ya Taarifa ya kikao iliyotolewa na Kiongozi Bwana Petronas Akili Yanga Afrika iliyosema:  HABARI WANA YANGA AFRIKA,KIKAO CHETU KITAFANYIKA 8/9/2012 MAHALI NI AFRICENTER MUDA NI SAA 9 MPAKA SAA 12 USIKOSE TAFADHALI,UWEPO WAKO NDIO KUFANIKISHA MALENGO YA GROUP.  Lakini jambo la kusikitisha wachangiaji wamekuwa niwachache sana.

Ni imani yetu kuwa kila mmoja atapitia taarifa hii ambayo imetolewa na mwanatanga.blogspot.com na kutoa maoni yake ili kujiridhisha juu ya idadi itakayoshiriki kwa ajili ya maandalizi ya Makabrasha ya Kikao. 

TAFADHALI MJULISHE MWANAGROUP MWINGINE
imetolewa na uongozi wa Yanga Facebook

No comments:

Post a Comment