MTANZANIA aliyejulikana kwa jina
moja la Patricia, mkazi wa jijini Dar es Salaam ambaye kwa sasa anaishi Texas,
Marekani hivi karibuni alijikuta akizua kasheshe nzito kufuatia kuanguka chini
na kurusharusha miguu kwa kile kilichodaiwa ni mapepo, Uwazi limepekenyua.
Katika DVD ya mahubiri ya mkutano mkubwa wa Kanisa la Synagogue Christian Of
All Nations ‘SCOAN’ la Nabii T. B. Joshua wa Nigeria ambaye alizuru nchini
Marekani hivi karibuni, Patricia alifika kuombewa kama waumini wengine lakini
cha ajabu mapepo yakampiga mwereka. Katika DVD hiyo, Patricia ambaye maandishi madogo chini ya DVD hiyo
yalithibitisha yeye ni Mtanzania aishiye Marekani, alianza kwa kumjia juu
Mtumishi wa Mungu, Wise Man Harry akitaka kupambana naye.
Hata hivyo, mtumishi huyo akilitumia jina la Yesu Kristo, alimmudu Patricia kiasi cha kumfanya aanguke chini kwa mwereka mzito kama mzigo huku kaumu ikimwangalia.Kabla ya mwereka huo, Patricia kupitia mapepo ‘yake’ alisema alimuua baba yake mzazi na kwa wakati huo alikuwa akitaka kumuua mama yake mzazi ambaye alikuwa kitandani akiugulia tatizo la ini.Akasema tatizo hilo yeye ‘pepo’ ndiye aliyeliingiza kwa mama wa Patricia kwa kuwa mwanamke huyo alikuwa akijifanya anaweza kusali kwa Mungu wake. Hata hivyo, baada ya kuangushwa na mapepo hayo kufuatia maombi ya Harry, Patricia alisimama na kukanusha yote aliyosema awali (kupitia mapepo).Alisema anampenda sana mama yake mzazi, hawezi kumuua na pia baba yake alikuwa mwema sana hivyo asingeweza kumuua kwa sababu yeye hana uwezo huo. Mtumishi Harry akamwambia roho chafu iliyokuwemo ndani mwake ndiyo ilikuwa ikisema hayo, imeshaondoka na hata mama yake yuko sawa maneno ambayo yalimfanya mrembo huyo kufurahi.
Katika mahubiri hayo, Wamarekani mbalimbali pia walipiga mwereka kwa mapepo ambapo baada ya kuombewa walirudia katika hali yao ya kawaida huku wakimshukuru sana Mungu.
KINYAIYA ATAPELI BUKU ISHIRINI
Na
Erick Evarist
MTANGAZAJI na mwigizaji maarufu
Bongo, Ben Kinyaiya amekwaa skendo ya kumtapeli Zeght Dibega ambaye alikuwa
mpangaji mwenzake, Mwananyamala jijini, Dar. Akizungumza na Motomoto Newz,
Zeght alidai kuwa, mwishoni mwa Julai, mwaka huu, alimpa Ben shilingi elfu 20
kwa ajili ya kununulia umeme na wakakubaliana endapo atahamishwa kwa kuwa muda
wake ulikaribia kuisha, basi Ben atachukua fedha hiyo kutoka kwa mpangaji mpya
na kumrejeshea yeye lakini hata alipohama, staa huyo hakufanya Hivyo. Alipotafutwa
Ben na kuulizwa kuhusu madai hayo alisema hivi:“Huyo dada ni mwongo mkubwa,
alishagombana na wapangaji karibu wote, mimi niliteuliwa kuchangisha fedha ya
umeme, nikafanya hivyo na umeme akautumia lakini nashangaa anadai nimemtapeli.“Yeye
pale alifukuzwa kwa sababu alikuwa haelewani na mwenye nyumba hadi wapangaji
wenzake,” alisema Ben.
WEMA NA SINURA NDANI YA BIFU
Na Mwandishi Wetu
KUKIWA hakujapoa vizuri baada ya ushoga wao kuvunjika, mwigizaji
wa sinema Bongo, Snura Mushi hivi karibuni alifanya mahojiano katika Runing a
ya EATV, Kipindi cha Hot Mix ambapo alianza dalili za kumvua Miss Tanzania 2006
na staa wa sinema za Bongo, Wema Sepetu ambaye aliwahi kuwa shosti wake mkubwa,
Amani linashuka nayo. Kwa mujibu wa macho ya mashuhuda, Snura alisisitiza kuwa, ana siri nzito za
Wema na siku akiamua kuzianika, basi mrembo huyo hatakatiza mitaani kwa aibu. Kwa maneno ya Snura, kila aliyetazama kipindi kile alisema hata kama mcheza
filamu huyo hakuzitaja moja kwa moja siri za mwenzake, lakini kila mtu anajua
Wema anatembea na aibu yake.
“Sasa kama Snura hakutaka kuzitaja hizo siri, kusema vile tu si tayari
ameshamuumbua mwenzake, kila mtu anajua Wema ana mambo mabaya,” alisema Nice,
mdada anayemiliki saluni moja iliyopo Kijitonyama, Dar.Kama hiyo haitoshi,
tayari Snura yupo kwenye mchakato wa kuandaa filamu inayoitwa Uozo wa Super
Star ambayo ndani yake ni Wema mwanzo mwisho. Filamu hiyo inaandaliwa na
Kampuni ya Chuz Entertainment ya Tuesday Kihangala ‘Chuz’.Habari nyingine
zinadai kuwa mara baada ya kumwagana na Wema, Snura kwa sasa amejipeleka kwa
Chuz ambako ameigiza baadhi ya ‘sini’ kwenye Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu
ambayo inaingia mtaani hivi karibuni
Wakati Snura akiwa na mengi ya moyoni, kwa upande wake, Wema
alitoa msemo wa Wahenga akimwambia Snura, Kimya Kingi Kina Mshindo. Alimtaka
Snura anyamaze na afute nia yake kwani yeye akianza kuzungumza ya kwake
anaamini Snura hataweza hata kutembea mitaani. “Nayasikia mengi sana anayozungumza Snura lakini mi ni muungwana, asinione nipo
kimya. Nikiamua kufunguka sitaweza kusikia la mnadi swala wala la muadhini. “Hakuna mtu asiyejua kama mimi ndiye nilikuwa naendesha maisha yake kama mke
wangu. Kila nguo nzuri anayoivaa kwa sasa au pochi anayobeba ni fedha zangu.
Namuomba kabisa asinichokonoe,” alisema Wema. Akaongeza: Nimeshamlipia kodi ya
nyumba Snura, nimeshamsaidia kulipa ada ya mtoto wake, sasa ni kwa nini
asiniheshimu?”
MAHABA YA DIAMOND NA MAMA YAKE TANGU KITAMBO
Na Sifael Paul
SIRI imefichuka! Kumbe mwanamuziki
‘anaye-hit’ kwa sasa katika muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond
Platinumz’ na mama yake mzazi, Sanura Khassim ‘Sandra’ walianza kupendana
zamani, Amani linashuka nayo. Kwa mujibu wa chanzo makini ndani ya familia
hiyo, Sandra ndiye aliyemlea Diamond na kupita katika vipindi vigumu kimaisha
baada ya baba yake, Abdul Jumaa kutengana na mama yake ndiyo maana mara nyingi
huwa wanaambatana hata kwenye shoo za msanii huyo ambazo kuna uwezekano wa
mzazi huyo kuhudhuria.
“Sandra ndiye aliyemsomesha Diamond
kwa shida hivyo hawezi kuacha kumpenda na ndiyo maana kila sehemu akiambiwa
awashukuru watu waliomfikisha hapo alipo, huwa mtu wa kwanza kumtaja ni mama
yake,” kilisema chanzo hicho na kuongeza: “Wewe msikilize Diamond, huwa anaanza
kumshukuru Mungu ‘theni’ anafuatia mama yake.”
Chanzo hicho kilitiririka kuwa kuna
wakati Diamond hata anasahau suala la kuoa kwa sababu anapata upendo wa kutosha
kwa mama yake. Hata mama yake naye ndiyo maana hawezi kuolewa kwa sababu tayari
kuna mtu wa kumfariji ambaye ana upendo wa dhati kwake. Sasa maisha yanataka
nini tena? Kwa mujibu wa Diamond mwenyewe, wakati anaanza kuhangaika kuchomoka kimuziki,
mama yake alikuwa akimpeleka kwenye ‘talent show’ hivyo mafanikio yake ni
dhahiri kuwa yeye ndiyo mwenye mchango mkubwa kuliko mtu yeyote hivyo hawezi
kuacha kumpenda daima.
WALIOFUMINIWA WAOANA
Na
Mwandishi Wetu, Arusha
SIKU chache baada ya gazeti ndugu
na hili, Risasi Jumamosi kuripoti juu ya fumanizi la babu mwenye umri wa miaka
70, Rafael Mitasio aliyenaswa gesti akiwa na mke wa mpangaji wake, taarifa
tulizozinasa zinadai kuwa mzee huyo amesusiwa mwanamke huyo. Chanzo chetu cha
habari kimedai kuwa, mara baada ya habari hiyo kutoka gazetini, mume wa
mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la baba Tausi aliumia sana hivyo akampa
kisogo kitendo kilichomfanya mgoni huyo atangaze kumuoa.
“Ile habari ilipotoka kwa kweli mume wa yule mwanamke aliumia sana, akaamua heri huyo mzee amchukue kabisa kama ameona anaweza kumtunza kuliko yeye. “Cha kushangaza yule mzee naye eti anadai wala habari hiyo haijamuumiza na anasema atamuoa kabisa mwanamke huyo ili kuwakata vilimilimi wabaya wake,” kilidai chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.
Kufutia taarifa hizo, Uwazi
lilimtafuta baba Tausi lakini hakuweza kupatikana mara moja. Mzee Rafael
alipotafutwa kuzungumzia kama kweli ana mpango wa ‘kumchukua jumla’ mwanamke
aliyenaswa naye wakivunja amri ya sita, alizungukazunguka sana lakini mwisho
akasema: ‘’Si mmeshaandika kuwa nimefumaniwa, haya kaandikeni tena kuwa nataka
kumuoa kabisa ili mfurahi.” Mzee Rafael
aliripotiwa kufumaniwa hivi karibuni kwenye gesti ya Sekei iliyopo mjini hapa
akiwa na mke wa mpangaji wake.
Tukio hilo liligeuka kuwa gumzo katika maeneo mengi ya mji huku wengi
wakishangazwa na kitendo cha mzee huyo kumshawishi mke wa mpangaji wake mpaka wakanaswa
wakiwa watupu gesti.
Hata hivyo, fumanizi hilo lilizua kizaazaa cha aina yake hadi likafikishwa
polisi.
JAMANI WATANZANIA TUMSAIDIE MTOTO HUYU
MTOTO Ashura Mustafa mwenye umri
wa miaka minne (pichani), mkazi wa Kijiji cha Mwandege wilayani Mkurunga, Mkoa
wa Pwani, yupo katika mateso makubwa kutokana na vidonda vilivyomtoka mwilini
na baba yake hana uwezo wa kumgharamia matibabu. Baba wa mtoto huyo, Mustafa
Mohamed, ana haya ya kusema: “Mtoto wangu alianza kuumwa akiwa na mwaka mmoja
baada ya kuzaliwa mwaka 2007. Vidonda hivi vilianza vikiwa ni malengelenge na
nimehangaika naye katika hospitali nyingi mpaka ikafika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. “Madaktari
Muhimbili walinipa barua ya kwenda CCBRT ambako wataalamu waliniambia kuwa
mtoto wangu huyu ana tatizo la saratani ya ngozi, ‘stage 4’.
Nikaambiwa mtu akiwa na saratani
hatua hiyo, vidonda vyake huchukua muda mrefu kupona.
“Ilitakiwa afanyiwe upasuaji lakini ikabainika kuwa hana damu ya kutosha, akapewa chupa mbili za damu lakini baada ya miezi miwili akapungukiwa tena. Akaongezewa tena chupa mbili lakini kabla ya kufanyiwa upasuaji, daktari aliyekuwa akimtibu CCBRT tukaambiwa amekwenda likizo, hivyo tukarudi nyumbani ambako yupo hadi sasa. “Mtoto wangu ana hali mbaya kwa kuwa anakaa ndani tu tena kwenye neti kukwepa vumbi na inzi, anateseka sana. Naomba msaada kutoka kwa wasamaria kwani sina kazi na kila tunapompeleka hospitali ni lazima tukodi gari. Hali aliyonayo hatuwezi kusafiri naye kwa daladala. “Aliyeguswa na mateso ya mwanangu awasiliane nami kwa simu namba 0769517765, 0715424607,” alisema Mustafa kwa masikitiko.

STAA bei mbaya wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond
Platnumz’ ameandika historia huko Washngton DC nchini Marekani kwa Rais Barack
Obama baada ya kuangusha shoo iliyojaa kufuru na kupagawisha Wabongo na watu wa
Afrika Mashariki waishio humo.
Tukio hilo lilijiri Jumapili ya Septemba 2, mwaka huu ambapo Diamond na ‘madensa’ wake watatu walikonga nyoyo za mashabiki wake waishio jijini humo na wengine kutoka katika miji jirani kama New York.
Akiwa stejini, Rais huyo wa Wasafi aligonga nyimbo zote za zamani na sasa na alipoona bado mashabiki wake wana mzuka…
KATIKA hali ya kushangaza, Mtangazaji maarufu Bongo, Lulu Mathias Semagongo
‘Aunt Lulu’ amefunguka kuwa atatimka nchini kwenda kuishi kusikojulikana.
Akizungumza na kona ya Mbovumbovu za Mastaa juzikati jijini Dar, Aunt Lulu alifunguka kuwa ameamua kukimbia mji kwani amechoshwa na manenomaneno ya walimwengu jijini. “Nimechoshwa kwa kweli na kwa kuwa mipango yangu ya kuchomoka imetimia, acha nitimke Bango angalau nikapumzike kidogo nje ya hapa,” alisema Aunt Lulu pasipo kutaja anakotimkia.
Alisema utafiti huo unafanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMRI), ulianza Machi mwaka huu na kwamba unahusisha wagonjwa 200 wanaofuatiliwa kwa kupimwa damu, kinga ya mwili (CD4) na uzito wa mgonjwa, ambao ulifanyika tangu mgonjwa alipokunywa kikombe cha babu. “Matokeo ya awali ya utafiti yameonyesha kuwa hakuna utofauti katika vipimo vya kimaabara pamoja na damu, CD4, uzito na ubora wa afya ya wagonjwa kati ya waliokunywa na wale ambao hawakunywa dawa ya mchungaji,” alisema Dk. Mwinyi. Alisema lengo la utafiti huo ni kubaini uwezo wa dawa hiyo katika kutibu magonjwa aliyosema dawa yake inayatibu ili kuona kama kuna utofauti wowote baada ya gonjwa kutumia dawa. Kufuatia hali hiyo, jeshi la polisi nchini limesema kwamba linafuatilia kwa makini sakata la Mchungaji Masapile anayeishi katika kijiji cha Samunge mkoani Arusha kufuatia malalamiko ya wananchi kuwa licha ya dawa yake kuonekana haitibu, bado watu wanakwenda na kunywa.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni ofisini kwake makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso, amesema kwamba kutokana na malalamiko hayo polisi watawasiliana na wizara ya afya ili kuchukua hatua stahiki.Msemaji huyo amesema kwamba wanataka kujua kama wizara ya afya imepiga marufuku dawa hiyo au inasema nini baada ya kubainika kuwa haitibu na amewataka wananchi kutoenda huko. Wananchi wengi waliozungumza na gazeti hili wamedai kwamba Babu amewatapeli wananchi na kinachowauma ni kuona kuwa kuna watu wanaendelea kwenda kunywa kikombe japokuwa hawatangazwi.
“Wananchi wengi waliuza mali zao na kukimbilia kwa babu kupata tiba, kumbe ulikuwa ni utapeli, ukweli ni kwamba serikali imechelewa mno kutoa tangazo hili,” alisema mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja tu la John. Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyama vya Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi nchini (TAMOPHA), Julius Kaaya, ameitupia serikali lawama kwa kuipigia debe dawa ya Babu na kuwafanya wagonjwa kutoroka hospitali huku wengi wao wakiacha kuendelea na dawa wakiamini wangepona baada ya kunywa kikombe kimoja .“Huyu Babu inatakiwa ashitakiwe apelekwe mahakamani afilisiwe mali zake zote alizochuma toka kwa wagonjwa na ikiwezekana afungwe ili iwe fundisho kwa watu wengine,” alisema Kaaya na kuongeza kuwa wao wanajiandaa kumfungulia kesi.
Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste (TAG) Mkoani Arusha, Steve Wambura, amemtaka babu huyo amrudie Mungu kwa kutubu kuwa aliwatapeli wananchi. Naye Mwenyekiti wa Waganga wa Tiba Asili Mkoa wa Dar es Saalam, Maneno Tamba, amesema babu huyo siyo mwanachama wao na walishangazwa na serikali kumpigia debe, hali iliyosababisha vifo vya watu wengi waliomkimbilia na kuacha tiba sahihi. Baadhi ya mawakili, akiwemo Mabere Marando wamesema kwamba wapo tayari kumfikisha mahakamani babu huyo wakijitokeza waliotapeliwa na watamfungulia kesi ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Tukio hilo lilijiri Jumapili ya Septemba 2, mwaka huu ambapo Diamond na ‘madensa’ wake watatu walikonga nyoyo za mashabiki wake waishio jijini humo na wengine kutoka katika miji jirani kama New York.
Akiwa stejini, Rais huyo wa Wasafi aligonga nyimbo zote za zamani na sasa na alipoona bado mashabiki wake wana mzuka…
Lulu Mathias Semagongo ‘Aunt
Lulu’.atimka bongo
Akizungumza na kona ya Mbovumbovu za Mastaa juzikati jijini Dar, Aunt Lulu alifunguka kuwa ameamua kukimbia mji kwani amechoshwa na manenomaneno ya walimwengu jijini. “Nimechoshwa kwa kweli na kwa kuwa mipango yangu ya kuchomoka imetimia, acha nitimke Bango angalau nikapumzike kidogo nje ya hapa,” alisema Aunt Lulu pasipo kutaja anakotimkia.
Stori:
Makongoro Oging'
SERIKALI imethibitisha kuwa
kitendo alichokuwa akifanya babu wa Loliondo, Mchungaji Ambilikile Masapile,
cha kutoa dawa ya kutibu magonjwa, ukiwemo Ukimwi aliyokuwa amedai kuwa
ameoteshwa na Mungu ni cha kitapeli. Utafiti umebaini kwamba dawa
hiyo ya babu wa Loliondo ni feki na kwamba haina uwezo wa kutibu Ukimwi
wala kisukari. Kwa mujibu wa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.
Hussein Mwinyi, utafiti wa kulinganisha wagonjwa wa Ukimwi na kisukari
waliokunywa dawa hiyo na wale ambao hawakunywa, umebaini kwamba hakuna utofauti
wa afya ya mgonjwa.
Alisema utafiti huo unafanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMRI), ulianza Machi mwaka huu na kwamba unahusisha wagonjwa 200 wanaofuatiliwa kwa kupimwa damu, kinga ya mwili (CD4) na uzito wa mgonjwa, ambao ulifanyika tangu mgonjwa alipokunywa kikombe cha babu. “Matokeo ya awali ya utafiti yameonyesha kuwa hakuna utofauti katika vipimo vya kimaabara pamoja na damu, CD4, uzito na ubora wa afya ya wagonjwa kati ya waliokunywa na wale ambao hawakunywa dawa ya mchungaji,” alisema Dk. Mwinyi. Alisema lengo la utafiti huo ni kubaini uwezo wa dawa hiyo katika kutibu magonjwa aliyosema dawa yake inayatibu ili kuona kama kuna utofauti wowote baada ya gonjwa kutumia dawa. Kufuatia hali hiyo, jeshi la polisi nchini limesema kwamba linafuatilia kwa makini sakata la Mchungaji Masapile anayeishi katika kijiji cha Samunge mkoani Arusha kufuatia malalamiko ya wananchi kuwa licha ya dawa yake kuonekana haitibu, bado watu wanakwenda na kunywa.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni ofisini kwake makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso, amesema kwamba kutokana na malalamiko hayo polisi watawasiliana na wizara ya afya ili kuchukua hatua stahiki.Msemaji huyo amesema kwamba wanataka kujua kama wizara ya afya imepiga marufuku dawa hiyo au inasema nini baada ya kubainika kuwa haitibu na amewataka wananchi kutoenda huko. Wananchi wengi waliozungumza na gazeti hili wamedai kwamba Babu amewatapeli wananchi na kinachowauma ni kuona kuwa kuna watu wanaendelea kwenda kunywa kikombe japokuwa hawatangazwi.
“Wananchi wengi waliuza mali zao na kukimbilia kwa babu kupata tiba, kumbe ulikuwa ni utapeli, ukweli ni kwamba serikali imechelewa mno kutoa tangazo hili,” alisema mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja tu la John. Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyama vya Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi nchini (TAMOPHA), Julius Kaaya, ameitupia serikali lawama kwa kuipigia debe dawa ya Babu na kuwafanya wagonjwa kutoroka hospitali huku wengi wao wakiacha kuendelea na dawa wakiamini wangepona baada ya kunywa kikombe kimoja .“Huyu Babu inatakiwa ashitakiwe apelekwe mahakamani afilisiwe mali zake zote alizochuma toka kwa wagonjwa na ikiwezekana afungwe ili iwe fundisho kwa watu wengine,” alisema Kaaya na kuongeza kuwa wao wanajiandaa kumfungulia kesi.
Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste (TAG) Mkoani Arusha, Steve Wambura, amemtaka babu huyo amrudie Mungu kwa kutubu kuwa aliwatapeli wananchi. Naye Mwenyekiti wa Waganga wa Tiba Asili Mkoa wa Dar es Saalam, Maneno Tamba, amesema babu huyo siyo mwanachama wao na walishangazwa na serikali kumpigia debe, hali iliyosababisha vifo vya watu wengi waliomkimbilia na kuacha tiba sahihi. Baadhi ya mawakili, akiwemo Mabere Marando wamesema kwamba wapo tayari kumfikisha mahakamani babu huyo wakijitokeza waliotapeliwa na watamfungulia kesi ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Na
Makongoro Oging'
NYUMBA ya msanii wa filamu Bongo,
Elizabeth Michael ‘Lulu’ (pichani) iliyopo maeneo ya Golani, Kata ya Saranga,
wilayani Kinondoni jijini Dar sasa imedoda kufuatia mwanadada huyo kuwa
gerezani akihusishwa na kifo cha msanii mwenzake, Steven Kanumba.Chanzo chetu
cha habari ambacho kinaishi maeneo hayo kililiambia Uwazi kuwa, kabla ya Lulu
kukutwa na matatizo hayo, ujenzi wa nyumba hiyo yenye vyumba sita ulikuwa
ukienda kwa haraka lakini sasa hivi umesimama.
“Kimsingi ile nyumba ya Lulu kule Golani imedoda, ujenzi unaenda kwa kusuasua sana tofauti na kipindi cha nyuma,” kilidai chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake na kuongeza: “Mwenyewe alikuwa akisema anataka kufanya haraka ili ahamie mwezi uliopita, ndoto zake zimeyeyuka, sasa imefikia kwenye linta na uendelezaji wake si wa kivile.”Baada ya kupata habari hizo, Uwazi lilifika maeneo ilipo nyumba hiyo na kufanikiwa kuiona ikiwa katika mazingira ya kudoda na lilipozungumza na mjumbe wa Tawi la Saranga, Bi. Cristina Emmanuel alisema: “Nyumba hii baada ya Lulu kufikwa na matatizo, mama yake ndiye aliyekuwa akija kuiendeleza lakini katika siku za hivi karibuni, ujenzi umesimama.”
Na
Gladness Mallya, Dar es Salaam
BAADA ya kuachana na mumewe
Hamisi Bwela, msanii wa filamu Bongo, Tamrina Posh ‘Amanda’ amenasa katika
penzi jipya kwa msanii wa Bongo Fleva, Joseph Rushalu `Bwana Misosi’.
Habari zilizopatikana kutoka katika chanzo chetu makini, zinasema kwamba,
wawili hao hivi sasa hawasikii wala hawaoni kutokana na kuzama katika penzi
motomoto. “Amanda amekufa ameoza kwa Misosi, sasa hivi mapenzi yao siyo siri tena... ni
njenje na wanapendana sana hakuna mfano kwa kweli,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizi Tollywood Newz iliwasiliana na Amanda ili kupata ukweli wa habari hizo ambapo bila hiyana alikiri kutoka na Bwana Misosi na kwamba anampenda kuliko maelezo.
“Ni kweli Misosi ni mpenzi wangu na ninampenda sana na sijui ni kitu gani kitakachonitenganisha naye,” alisema Amanda.
Stori: Musa Mateja na Shakoor Jongo
MISS aliyetwaa nafasi ya 2, 2012 katika shindano
maalum la mwaka huu, Hamisa Hassan, anadaiwa kuichafua Miss Tanzania
kufuatia kwenda kushiriki kinyemela Shindano la Miss University Africa 2012
nchini Nigeria hivi karibuni.Ilidaiwa kuwa ili mrembo ashiriki shindano hilo,
linalopokea walimbwende kutoka barani Afrika, lazima atoke kwenye moja ya vyuo
vya nchini mwake sifa ambayo Hamisa hakuwa nayo.
Ilibidi mapaparazi wetu wamsake Mkurugenzi wa
Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga ‘Anko’ ili atoe ufafanuzi kuhusu madai
hayo hasa ikizingatiwa kuwa, katika shindano maalum la hivi karibuni, Lissa
Jensen aliibuka kidedea na Hamisa kushika nafasi ya pili. “Ni kweli Hamisa ni
miss wangu, lakini utaratibu wa kwenda Nigeria kushiriki shindano hilo sifahamu
aliutoa wapi? Najua hakuna chuo chochote anachosoma kwa sasa na wala hakuna
mashindano kama hayo kwangu,” alisema Lundenga.
Kwa upande wake, Hamisa alipobanwa ili kutoa
maelezo kuhusu tuhuma hizo alikiri kutosoma chuo chochote nchini. Aidha,
alikiri kushiriki shindano hilo huku akisema kuwa hayupo tayari kuwataja
waliomchagua. “Ni kweli sisomi chuo chochote ingawa nina mpango huo, ni kweli
nilikuwa Nigeria kushiriki Miss University Africa 2012 na niliingia top ten,
lakini taji lilichukuliwa na mshiriki kutoka Lesotho (pichani chini), lakini
siwezi kuwataja walionichagua kwenda,” alisema.
AJALI MBAYA WAKATI WA IDDI
No comments:
Post a Comment