Tasisi
ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Nchi za Kusini mwa Afrika (MISA Tan) imepokea
kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mwandishi na kiongozi mahiri wa
waandishi hapa nchini.
Aidha
tunaungana na waandishi na wafanyakazi katika tasnia ya habari nchini, Jumuiya
ya Klabu za Waandishi nchini (UTPC) pamoja na familia ya marehemu Mwangosi
katika kipindi hiki kigumu ambacho tasnia yetu ya habari imelazimika kuingia
matatani kutokana na matumizi ya mabavu ya Jeshi la Polisi.
Tunalaani
kwa nguvu zote matumizi ya mabavu ya polisi ambayo yamesababisha kifo cha
mwandishi wa habari akiwa kazini na pia akiwa chini ya ulinzi wa Polisi.
Tunatambua
uhasama kati ya Polisi wa mkoa wa Iringa dhidi ya waandishi wa habari uliodumu
kwa muda mrefu.
Uhasama
huu kiini chake ni kutokana na matumizi ya nguvu kupita kiasi yanayotekelezwa
mkoani Iringa na hivyo kila mara waandishi wanaporipoti habari wanaingia katika
mlolongo wa uhasama na vituko vya mara kwa mara.
Hatimaye
polisi kwa makusudi wameamua kuua mwandishi. Hili ni doa ambalo litaichukua
Tanzania kujisafisha machoni pa jumuiya ya kimataifa.
Huu
ni mwendelezo wa matumizi ya nguvu kupita kiasi yanayofanywa na polisi kwa raia
wa nchi hii. Ni lini polisi watasimamia ulinzi wa raia na mali zao badala ya
kugeuka kuwa jeshi la mauaji kila wananchi wanapokusanyika kwa minajili ya
kutimiza ndoto zao?
Kifo
cha Mwangosi kimegubikwa na sintofahamu hasa ukijua kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Iringa Bwana Michael Kamuhanda alikuwa anamtambua kama kiongozi wa waandishi
wa habari mkoa na alikuwepo kwenye tukio wakati Mwangosi akiwa mikononi mwa
polisi, na kuuliwa mbele yake.
Lakini
ikumbukwe kuwa siku zote hata katika vita waandishi wanafanya kazi bega kwa
bega na askari ili kuwajuza wananchi nini kinachotokea kwenye uwanja wa
mapambano.
Kwa
jeshi la polisi hapa nchini limedhihirisha kuwa 2 baada visa na mikasa
kuwatokea raia wa kawaida sasa wamewageukia waandishi wa habari na kukatisha
maisha yao kikatili.
Sasa
Polisi wamevunja daraja lililokuwa linawanganisha wananchi na serikali yao. Hii
itazidisha chuki ya wananchi dhidi ya serikali yao kuliko kipindi kinginecho
chote.
Ikumbukwe
pia kuwa wakati mauaji haya yanatokea kuna mkutano mkuu wa UTPC unaoanza wiki
hii huku wawakilishi wa vyama vya waandishi wa mbalimbali wa kimataifa
wakitegemea kushiriki katika mkutano huo wa mwaka.
Na
hii itatoa taswira halisi ya jinsi Jeshi la Polisi linavyofanya kazi hapa
nchini.
Jumuiya
ya kimataifa itaweza kujionea hali halisi jinsi waandishi wa habari hapa nchini
wanavyofanya kazi katika mazingira hatarishi na kwamba sasa Tanzania inawezekana
isiwe mahali salama pa kuishi kama walivyokuwa wakisikia kwenye vyombo vya
habari vya kwao. Mfano halisi ni mhanga Daudi Mwangosi ambaye ataingia katika
vitabu vya kumbukumbu duniani kwa mwaka 2012.
Tunaiomba
serikali ichukue maamuzi makini ya kukaa pamoja na vyama vya siasa ili kutafuta
njia muafaka ya kutuliza mikusanyiko ya wananchi kwa njia za amani na sio
kutumia mabavu katika kuwatawanya.
Ni
imani yetu kuwa historia imeonyesha kuwa nguvu kupita kiasi kwa wananchi
inaongeza chuki dhidi ya serikali yao ya wakati huo na kamwe hainyamazishi
dukuduku
zilizoko mioyoni mwa wananchi. Kokote kule duniani matumizi ya polisi
yalipovuka mipaka yakaamsha hasira za wananchi na kuzifanya nchi hizo
zisikalike.
Matumizi
ya mabavu, nguvu kupita kiasi kuzima vuguvugu za wananchi kwa kile
wanachokiamini pamoja na mauaji na hasa kwa wanahabari na raia wasio na silaha
hayajawahi kufanikiwa kokote kule duniani.
Tunaamini
kuwa serikali yetu ni sikivu na itachukua hatua stahiki. Pamoja na kwamba
uchunguzi huru sio utamaduni wa serikali yetu lakini katika hili la mwandishi
akiwa na kalamu na kamera yake afie mikononi mwa polisi tunahitaji uchunguzi
huru na wa kina.
Taasisi
yetu imetoa ubani wa shilingi laki tano (500,000) kwa familia ya marehemu
Mwangosi. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Amen!
Tumaini Mwailenge
Mkurugenzi,
MISA Tanzania
No comments:
Post a Comment