![]() |
KARDINAL RUGAMBWA |
Kanisa katoliki nchini Jimbo la Bukoba Mkoani Kagera, wanajiandaa
kuzika upya masalia ya mwili wa aliyekuwa askofu wa Jimbo la hilo Kardinali
Laurean Rugambwa, aliyefariki mwaka 1997 katika kanisa kuu la Bukoba.
Maziko ya Kadinali Rugambwa yamepangwa kufanyika siku ya oktoba 6 mwaka
huu. Mwili wa askofu huyo wa kwanza nchini na Kardinali wa kwanza mweusi barani
Afrika umezikwa katika kanisa la kwanza mkoani Kagera lililopo Kashozi kutokana
na kwamba kanisa kuu la Bukoba ambalo marehemu aliagiza kuzikiwa ndani yake
lilikuwa katika matengenezo makubwa.
Askofu msaidizi wa
Jimbo la Bukoba Askofu Methodius Kilaini , amesema wanataka kumzika kardinali
Rugambwa kwa heshima tena katika kanisa alilopenda kuzikiwa kutokana na
kukamilika kwake, lakini kabla ya kuzikwa humo kutatanguliwa na ibada
mbalimbali ikiwa sehemu alikozaliwa, alikobatizwa, sherehe zitakazoambatana na
kusherehekea miaka 100 ya kuzaliwa kwa kardinali Rugambwa tarehe 7 mwezi
Octoba.
Kanisa kuu katoliki jimbo la Bukoba ambalo masalia ya mwili wa marehemu kardinali Rugambwa yatazikwa ndani yake. |
"tuna alika watu wengi kuhudhuria kwenye tukio hili..., na
pia tunakaribisha michango itakayowezesha kuwa na kitu cha kumkumbuka marehemu
kwa mchango wake.... alisema askofu Kilaini. Naye mmoja wa wajumbe wa kamati ya
maandalizi ya kufanikisha tukio hilo , James Rugemalira, alimwelezea Kardinali
Rugambwa kama mtu aliyetoa mchango mkubwa kwenye jamii ya watanzania, kuanzia
kwenye nyanja za elimu, afya na kiroho.
Marehemu Kardinali Rugambwa ana mambo mengi ya kukumbukwa na
jamii ya watanzania hususani watu wa mkoa wa Kagera hasa kwa juhudi zake za
kupeleka elimu mkoani humo kwa kuagiza ujengwaji wa shule za msingi na
sekondari ikiwemo shule ya kwanza ya wasichana ya Rugambwa ambayo ujenzi wake
ulikuwa ni mafanikio ya marehemu huyo kuomba msaada wa ujenzi wa shule hiyo
alipohutubia bunge la Ujerumani akiwa mwafrika wa kwanza.
Licha ya mambo hayo yote kanisa hilo pia liko mbioni kuanzisha
mfuko rasmi wa kumuenzi kardinali huyo mfuko utakaojulikana kwa jina la
Kardinali Rugambwa ambao utakuwa maalumu kwa ajili ya kufanya shughuli
mbalimbali za kijamii.
Padre Laurean Rugambwa aliwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 10
Februari,1952. Alizaliwa julai 22 1912 na kufariki miaka 15 iliyopita.
No comments:
Post a Comment