na Bertha Mwambela, Muheza
HALMASHAURI
ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga inakabiliwa na ukosefu wa walimu na
madaktari, na kwamba hali hiyo imesababisha kudorora kwa sekta ya elimu
na afya.Kauli
hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza,
Amir Kiroboto wakati wa kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani kwa
mwaka wa fedha 2011/2012.
Alisema
ukosefu huo wa rasilimali watu katika idara hizo mbili nyeti ni wa muda
mrefu kwa zaidi ya miaka minne mfululizo, hivyo kuwafanya washindwe
kufikia malengo katika utendaji wao wa kazi.“Inanisikitisha
kuona kuwa ni zaidi ya miaka minne mfululizo tumekuwa na tatizo hili,
shule tunazo, zahanati pia tunazo, lakini hazina madaktari. Kwa kweli
inaumiza sana, hivyo inabidi kwa umoja wetu tusaidiane katika kupunguza
au kumaliza kabisa tatizo hili,” alisema Kiroboto.Aliwapongeza
madiwani na watendaji wa halmashauri hiyo kwa kusimamia vizuri majukumu
yao na hivyo kusababisha halmashauri hiyo kupata hati safi mara tatu
mfululizo.
Alisema
anaamini kuwa mshikamano, upendo na umoja ndiyo nguzo pekee iliyoweza
kuwafikisha hapo walipo kwa sasa kwa kuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) amekuwa akifanya kazi bila ya kukutana na tatizo lolote
katika halmashauri hiyo.Nae
Mkuu wa Wilaya hiyo, Subira Mgalu aliwataka madiwani kutimiza vema
wajibu wao wa kuwatumikia wananchi katika maeneo yao ya kazi, kwani kwa
kufanya hivyo kutasaidia kuwanyima nafasi wapinzani katika kuikosoa
serikali, ambao alisema kwa sasa anawafananisha na walimu katika
kufuatilia mambo yanayohusu jamii kwa ukaribu.
“Naamini
kuwa siasa za sasa zimebadilika hivyo madiwani tuwe makini katika
utendaji ili tuwanyime nafasi wapinzani wetu ambao wao muda wote
wamekuwa makini kutufuatilia na kuikosoa serikali iliyoko madarakani,”
alisema Mgalu.
No comments:
Post a Comment