Jina lake
kamili ni Alain Kahanga
Dekula , alizaliwa katika jimbo la Kivu katika Jamhuri ya Kongo. Baada ya
kumaliza High School alianza kupiga gitaa katika bendi ya Bavy National
iliyokuweko Uvira Kusini mwa Kivu. Baadae akiwa na kaka yake Rachid King
wakajiunga katika bendi ya Grand's Mike Jazz Band wakati huo ikiwa na
wanamuziki kama Remmy Ongala, Kasaloo Kyanga,
Kyanga Songa na Kawele Mutimanwa. Akaja Tanzania na kujiunga na Orchestra Maquis
Original na kati ya nyimbo ambazo anajulikana nazo sana ni Ngalula na
Makumbele. Wakiwa na mtindo wa Zembwela-Sendema, alikuwa jukwaa moja na miamba
wa magitaa wakati huo akina Nguza Viking "Big Sound" na marehemu
Ilunga Lubaba. Vumbi kwa sasa yuko Sweden
akiwa na yule mwanamuziki maarufu toka Uganda Sammy Kasule wakiwa na bendi ya
Ba makonde wamekwisha toa album CD mbili- Bamakonde na Asante.
Akiwa na bendi ya kaka yake Rachid King Orch Grand’s Mike wametoa album ya CD
Bolingo Ekeseni.
Kwa wapenzi wa Maquis Original jina la
"Vumbi" ni la kutia kumbukumbu nyingi sana,
na kwa wale ambao wamekuwa wakiusikia ule wimbo wa Chatanda Ngalula walisikia
tena na tena Tchimanga Assossa akilitaja jina hilo
wakati Vumbi anacharaza gitaa tamu la solo kwenye wimbo huo.
No comments:
Post a Comment