BM BARBERSHOP KINONDONI

Sunday, September 2, 2012

USIMUONE KOBE KAINAMA UJUE ANATUNGA SHERIA… MAONYESHO MATATU YA WATU MAKINI KWA WANAMUZIKI MAKINI



 













Safari ya Muziki inahitaji Uvumilivu wa hali ya juu sana. Muziki wa Dansi umeingia katika hatua nyingine kwasasa baada la wimbi la Wanamuziki kuamka usingizini na kulilia Maslahi kwa faida ya maisha yao. Ni kweli kuwa huwezi kufanya kazi mahali ambapo hakuna maslahi, lakini pia huwezi kuwa na maslahi yasiyo na TIJA kwenye Kazi yako.

Lilia maslahi na fanya kazi ionekane. Roma ni mji mkuu na mashughuli sana nchini Italia lakini haukujengwa kwa siku moja. Kuna dhana nzuri ambayo kwasasa imeenea kwenye vinywa vya kila Mwanamuziki kulilia maslahi. Wadau makini waliona kweli saa ya Ukombozi kwa wanamuziki sasa imefikia mahali pazuri sana. Kibaya zaidi ni pale ulaghai unapopenya kwenye NYOYO za wale wanaoona kuwa muziki utakuzwa kwa Pesa bila Vipaji. Usajili wa aina yoyote unaozingatia biashara au Faida haufanywi bila Mipango. Hakuna biashara ngumu kama ya Muziki au Mpira, unapojiingiza kwenye biashara hizi nilazima ujipange sana na ujue kuwa kuna kukosa na kupata na huwezi kupata faida kabla ya miaka minne hadi mitano ya KUKUBALI kupoteza hasa ukiwa umeingia kwa DHANA ya FEDHA. 

Unapokuwa na fedha na ukaonyesha WALAFI kuwa FEDHA ipo kila mtu takuwa rafiki yako na watatokea MAGUNDI wa kukufundisha jinsi ya kutumia FEDHA yako uliyoitafuta Mwenyewe. Hivi inakuwaje wewe ufundishwe kutumia Fedha ambayo uliitafuta mwenyewe??? Kila mtu ana njaa hivyo atatafuta jinsi ya kumfanya mwenye Fedha atoe pesa yake kwa Ulaghai ili afaidi yeye.

Maneno yangu yanaweza yakawa SUMU au CHACHU kwa wale wenye uelewa wa mbali. Kwa biashara kubwa kama hii ya Muziki inayowahusisha watu ambao tayari wanaijua kazi yao ni ngumu sana hasa pale wanapojazana kwa dhana ya kutengeneza pesa zaidi kuliko kazi. 

SWALI NAULIZA:
Hivi uwekezaji wa Mamilioni ya Fedha yanayosimamiwa na mtu aliyeishia Darasa la Saba ambaye hata kuhesabu moja mpaka kumi anajifikiria mara kumi inawezekana kweli ukampa jukumu la kusimamia mamilioni yako wakati hata neon :BUSINESS PLAN” halijui?? Naogopa sana na ninachelea kusema kuwa nyie mliojaaliwa na Mungu kupata fedha zenu na mnayo nia nzuri ya kuwainua hawa Wasanii wa Muziki jiulizeni kuwa tangu mlipowekeza mmeweza kurudisha japo theluthi ya mlichotoa?? Kama bado je mnatarajia kitarudi baada ya muda gani??? Mipango hiyo ipo??? Au mnasikiliza MILUZI??/ Hamjachelewa jiulizeni tena Miziki si lelemama.

TWANGA YAJIPANGA UPYA KWA KUMREJESHA KALALA JR.
USIKU wa kuamkia Jumamosi katika Ukumbi wa Mzalendo Pale Kijitonyama  Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’ ilikuwa ikimkaribisha Mwanamuziki Kalala Junior ambaye aliondoka mwaka mmoja uliopita kwenda kutafuta maisha na Bendi ya Mapacha Watatu. Baada ya kutafuta kwa muda huo amerejea nyumbani alikokuwa Twanga Pepeta na kusema kuwa amejifunza mengi huko nasasa ameamua kutulia fanye kazi. Jambo hili linaonyesha kuwa huko hakuna mapya zaidi ya kutojipanga na Ukurupukaji wa Wanamuziki,. Nderemo na vifijo kutoka kwa mashabiki vilizizima baada ya Mwanamuziki huyo kutoa historia ya Safari yake kupitia kwenye Wimbo wake Mpya aliokuja nao unaojulikana kwa jina la NYUMBANI NI NYUMBANI.  
 
 





No comments:

Post a Comment