Katika kipindi cha mwisho cha miaka ya 80, Kinondoni
ilkuwa inawaka moto kwa Vijana siku ya Jumapili. Lang'ata ambayo baadae ilikuja
kuwa Club ASET na sasa kanisa, palikuwa ndo ukumbi wa Dansi za kuanzia mchana
kwa Bendi ya Maquis. Ukija hapa mbele Vijana Jazz Pambamoto awamu ya pili chini
ya uongozi wa Hemed Maneti walikuwa nao kila Jumapili mchana wanaporomosha
Dansi, na siku hiyo ilipewa jina Vijana Day.
Kwa kweli Maquis walikuwa wanajaa watu na
Vijana wanajaa watu. Kulikuweko na wapenzi wa kudumu wa Vijana kama ilivyokuwa
Maquis. Wakati huo nyimbo kama Ngalula, Makumbele zilikuwa zinalia Lang'ata
huku Vijana wanateremsha Shingo feni, Ngapulila, Azda. Ushindani huu
ulilazimisha bendi kujitahidi kupiga vizuri na kwa displine au la wapenzi
wanahamia bendi jirani. Kuna wakati Vijana Jazz walikuwa wanaanza muziki saa
kumi na moja jioni na kupumzika saa tatu na nusu usiku kisha kumaliza dansi saa
nne.
Maquis wakawa wanaanza saa kumi na kumaliza
saa tano usiku. Na wakaanza kuruhusu mtu yeyote atakayekuwa kapigwa muhuri wa
kuruhusu kutoka nje ya ukumbi Vijana Jazz, aliruhusiwa kuingia Maquis bure.
Vijana wakabadili ratiba na kuanza kupiga saa 9 mchana, kwa mtindo wa bandika
bandua, yaani muziki nonstop. Na kufuta kupumzika hadi saa tano. Hiyo ndo
ilikuwa raha kwa wapenzi. Vijana haikuwa na show wakati wa Maneti, Lakini show
ilikuja baadae katika kukabili show ya Maquis ambayo ilikuwq nzuri sana chini
ya mwalimu wao Wabangoi. Majina makubwa yalitawala madansi hayo Maquis kulikuwa
na Dekula Vumbi kwenye solo,second solo Mbwana Cox (aliyetoka Vijana Jazz), banza
Mchafu Bass, Nguza Viking, Adios, Tshimanga Assossa,Parashi Lukumbule Vijana
Jazz kulikwa Shaaban Wanted, Hemed Maneti, Eddy Sheggy, Adam Bakari, Kida
Waziri, Abou Semhando, Rashid Pembe na wengine wengi, basi raha kila jumapili
ilikuwa kama tamasha
No comments:
Post a Comment