Jeshi la polisi mkoani Arusha linamsaka aliyekuwa mmbunge wa
jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kwa tuhuma za kushambulia mwili pamoja na
upotevu wa simu pamoja na fedha. Akiongea na waandishi wa habari jijini
hapa kamanda polisi Lebaratus Sabas alisema kuwa jeshi la Polisi
linamsaka Lema na wenzake ambao idadi yake hawajatajwa kwa tuhuma za
kushambulia mwili wa watu wawili tukio lililofanyika Oktoba 28 mwaka huu katika Kata ya Darajambili.
Alisema kuwa jeshi la Polisi lilipokea taarifa za
malalamiko kutoka kwa watu wawili waliojulikana kwa jina la Ibrahimu Juma
pamoja na Maritin Daniel wote wakazi wa darajambili kuwa aliyekuwa mbunge wa
jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiwa na wanzake walimvamia na
kuwashambulia kwa ngumi pamoja na kuwanyanganya simu aina ya samsung yenye thamani
ya shilingi laki tatu pamoja na fedha taslim kiasi cha shilingi laki mbili
kisha kuondoka na kuwaacha. Alisema kuwa watu hao waliamua kutoa taarifa polisi na polisi
inamsaka Lema kwa ajili ya kujibu tuhuma hizi .
No comments:
Post a Comment