Meneja wa Band ya Mapacha watatu Hamic Dacota
anatarajia kuanza kurusha Kipindi cha X-Africa kuanzia Jumamosi hii kupitia
Television ya DTV kila siku ya Jumamosi kuanzia saa moja usiku.
Akiongea na Mwanatanga Hamis Dacota ambaye kwa
taaluma ni Mwanahabari ameamua kuanzisha kipindi hiki ili kufufua Muziki wa
dansi ambao kwasiku za karibuni umeonekana kumezwa na muziki wa Bonngo Flava
ambaye yeye anauita Muziki wa Kuongea na siwa Burudani. Kama kawaida ya Hamis
huwa ni mcheshi na mtu wa Utani ametumia kauli Mbiu ya BACK TO MY
PROFFESSIONAL.... kuonyesha kuwa haachani na Umeneja wa Mapacha Watatu la Hasha
ila ameona ni vyema pia akatumikia Taaluma yake ya Utangazaji kupitia Kipindi
hiki ambacho kwasasa ni Gumzo la Jiji.
Dacota amenukuliwa na mwanatanga akisema kuwa “Najua nini mnahitaj na kwa muda mrefu mlikosa mtu wa kuwapa
burudani hizo, hakuna bongo flava humu ambazo wanazilazimisha watangazaji
wengine kuita muziki
wa africa..hapa ni band za Tanzania ..congo..Coupe de kale Africa Magharibi
kina Yousoundour..Manu Dibango wes, djako..keita..yaani wenge kofie,f ally
werason, jb and many more bila kusahau zile classic swedeswede....”
Mdau mmoja maarufu bwana Gerald amemuasa Dacota kwa kusema
kuwa “ Ukweli sisi walaji tunahitaji ladha mpya na nzuri ambayo tumekuwa
tukiikosa kwa muda mrefu naamini Dakota umejipanga vizuri na tambua tuna
mategemeo makubwa kutoka kwako...bro Mwanatanga na kubaliana na wewe kabisa kuwa muziki wa kiafrica
sasa utakuwa umepata muarobaini...tuko bega kwa bega kuhakikisha X-africa
inakuwa moto....
Aidha Dacota alitania na kusema ”Kaka deo ww ni mdhamini
mkuu wa kazi yangu najua upokifua mbele kunilinda kunisemea..ahadi yangu kwako
sintokuangusha nakuahidi mabadiliko na balance to perfection kwa kazi yooote
..kila kikundi mwanamuziki ana haki sawa hakuna upendeleo..nipo kikazi zaidi tuombe
uzima show itakua kila jumamosi saa moja jioni ..kuna vipengele vitatu muhimu
..interview na wadau wa burudani ya kiafrica..interview na ma dancerz tu wake
kwa waume..na wanamuziki ama band kwa ujumla ..habari za nini kinachoendelea katika
tasnia hii ya muziki wa kiafrica. Yaani dance..coupe de kale..miduara,, na kila
aina ya muziki wa kiafrica bongo flava haihusiki kabisa..uchambuzi wa kina
..mambo mengi mazuri mtayaona tusubiri tafadhali!!!.
Mwanatanga inaishi kwa kuamini kuwa huyu Dogo anaweza kuwa
Mkombozi wa Miziki ya dansi.l
No comments:
Post a Comment