William Godfrey Mhando |
Taarifa iliyotolewa na bodi ya
Wakurugenzi Tanesco imesema kutokana na tuhuma mbalimbali za ukiukwaji wa
taratibu za shirika ikiwemo matumizi mabaya ya mamlaka, julai 16 2012 bodi
iliamua kumsimamisha kazi Mkurugenzi mtendaji Mhandisi William Mhando pamoja na
maafisa wengine waandamizi ili kupisha uchunguzi huru na wa haki ili kufahamu
ukweli wa tuhuma hizo.
Baada ya hapo ofisi ya mdhibiti
na mkaguzi mkuu wa hesabu za mashirika ya Umma ilifanya uchunguzi ili kujua
ukweli juu ya tuhuma zilizokua zinamkabili Mhando ambapo katika uchunguzi huo
mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za mashirika ya Umma aligundua kuwepo kwa
ushahidi dhahiri wa ukiukwaji wa taratibu za shirika na matumizi mabaya ya
madaraka dhidi ya Mkurugenzi mtendaji mhandisi William Geofrey Mhando.
Baada ya kupokea ripoti ya
mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za mashirika ya Umma, bodi iliteua jopo la
watu watatu kusikiliza utetezi wa mhandisi Mhando dhidi ya tuhuma mbalimbali
zilizoibuliwa na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za mashirika ya Umma ambapo
baada ya kumsikiliza jopo hilo lilimkuta mhandisi Mhando na hatia ya makosa
yanayohusiana na ukiukwaji wa taratibu za shirika ikiwemo mgongano wa kimaslahi.
Pamoja na yote yalioelezwa,
tarehe 29 October 2012 bodi ilikutana na kujiridhisha kwamba mhandisi Mhando
alifanya makosa yanayohusiana na kuingia kwenye mikataba yenye mgongano wa
kimaslahi kinyume na taratibu za shirika ambapo kufatia makosa hayo bodi ya
Wakurugenzi imeamua kumwachisha kazi Mhando kuanzia tarehe 29 oktoba 2012.
No comments:
Post a Comment