NI kivumbi! Kuna madai kwamba, staa
wa Bongo asiyechuja, Wema Sepetu amemfikisha mama yake, Miriam Sepetu
kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar kwa madai ya kwenda
nyumbani kwake na kufanya vurugu zilizosababisha kuharibika kwa samani
mbalimbali, Ijumaa limeinyaka.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, ishu hiyo ilijiri usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, jijini Dar.
Mbali na mama mtu, wengine
waliofikishwa kituoni hapo ni dada mkubwa wa Wema aitwaye Nuru na kijana
aliyefahamika kwa jina moja la Bestizo ambaye inasemekana ni mshirika
mkubwa wa Diamond kwenye masuala ya mtandao wa msanii huyo.
“Wema alikuwa nyumbani kwake usiku
huo, watuhumiwa hao wakamzukia na kuanza kumchapa makofi ya ‘kelbu’
ambapo katika mshikemshike huo, baadhi ya vitu vilivunjika na kumtia
hasara staa huyo,” kilisema chanzo.
Haikujulikana mara moja ni kitu gani
kilisababisha mama mzazi huyo, dada mtu na kijana asiyekuwa ndugu kwenda
kwa Wema na kutenda kosa hilo.
Wema alikwenda polisi na kuandikisha
maelezo ambayo yameingizwa kwenye jalada lenye kumbukumbu;
KJN/RB/2755/2013 SHAMBULIO, KUHARIBU MA
No comments:
Post a Comment