Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka amerejea Usiku wa kuamkia leo akitokea Nyumani kwa Kigoma. Mwanamama huyu wa kimanyema aliondoka siku kadhaa zilizopita kuelekea nyumbani kwao alikozaliwa KIGOMA NI MUJI.
Kitu cha ajabu nikwamba mwanamama huyu aliondoka peke yake kwa Gari aina ya Lexus akiwa anaendesha bila usaidizi wa mtu yoyote kwa safari zote za Kwenda na Kurudi Kigoma. Umbali wa kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma ni Takribani Kilomita 1450 jambo ambalo limenishangaza sana na ninaamini hata wengine litawashangaza Pia. Akiongea na Mwanatanga Asha baraka amesema kuwa yeye ni Zaidi ya Mwanamke na sasa amerejea akiwa Kamili baada ya KUFUNDWA na wazee wa KIMANYEMA. Ameahidi kuudhihirishia Umma kuwa yeye ni mama mwenye Mtazamo wa mbali na atawadhihirishia watu hili kuanzia kwenye Show yake ya Kumkaribisha Mtoto wake Kalala siku ya Ijumaa pale Mzalendo Pub Kijitonyama.
No comments:
Post a Comment