BM BARBERSHOP KINONDONI

Wednesday, August 29, 2012

KWELI DUNIA RANGIRANGIRE MAMA NA MTOTO WAFUNGA NDOA BAADA YA BABA KUFARIKI

Hawa ni Mama na Mwana waliofunga ndoa Huko Namtumbo Songea

MARA kadhaa kumekuwa kukijitokeza matukio mbalimbali ya Kustaajabisha, Kusikitisha, Kushtusha, Kuhuzunisha na Kutisha na mengine yakihisiwa kuwa ni imani za kishirikina na mara nyimgi matukio ya aina hii hayo hutokea hata hapa nchini kwetu Tanzania na kuzua maswali mengi yanayo kosa majibu.

Katika Mkoa wa Ruvuma kuna tukio la kufungia Karne lililowastaajabisha wakati wa Mkoa huo na kuwafanya watu kutoamini kile wanachokisikia na hata wale waliyoshuhudia kutoamaini macho yao. Tukio hili linakuwa kama limegubikwa na imani za KISHIRIKINA kwakuwa siyo la kawaida kutokea kwenye Jamiii ya Watanzania kulingana na Imani zetu. Wahusika wote Kwa pamoja wametanabahisha kuwa wamefanya Kwa RIDHAA yao hivyo si sahihi wakaingiliwa kwenye jambo hili japo tendo lenyewe si sahihi Kwa Itikadi za Kidini, Kimila na hata Destuli za mtanzania.

Tukio linalozungumzwa limefanywa na Mama na Mtoto ambao majina yao ni Mama Condorada Ngonyani (70)  mkazi wa mkoani Ruvuma aliyeamua kufunga ndoa na mtoto wake wa tatu wa  kiume wa kumzaa na kuishi naye kinyumba kama mke na mume. Jambo hili limewashangaza sana majirani zao na Jamii kwa ujumla Wananchi wapatao 400, wa mkoa walijitokeza kushuhudia kioja hiki kwenye Mkutano wa Kijiji uliyoitishwa na Uongozi wa Serikali ya Kijiji walipoamua kuwafuatilia na ili kuwahoji juu ya jambo hili. Wanakijiji waliweka hadharani  jambo hili na kuuomba uongozi wa Mkoa wa huo na Wizara ya Maendelo ya Jamii, Jinsia na watoto, kufuatilia kwa karibu suala hilo na kuwaondoa hofu wananchi juu ya uhalali wa jambo hili Kisheria la Mtoto na Mama Mzazi kuweza kuishi kinyumba tena kwa NDOA halali.

Mama Condorada Ngonyani alisema kuwa mara baada ya kufariki mume wake, Mzee Mapunda aliamua kumchagua mtoto wake wa tatu kwenye uzao wake  ndugu Joseph Mapunda ili amrithi baba yake katika kuumiliki mwili wake kama ambavyo alikuwa akifanya Baba yake mzazi enzi za uhai wake ili kuondokana na tamaa na vishawishi vya Kimwili. Baada ya uteuzi huo walifunga ndoa ya kimila japo kuna baadhi ya wanafamilia hawakufurahishwa na tukio hilo, lakini yeye aliamua kutia pamba masikioni na kuamua kuvunja amri ya sita na mtoto wake wa kumzaa. Tukio kama hili ni mara ya kwanza kutokea mkoani Ruvuma nakwa Tanzania nzima. Tukio hili limeacha maswali mengi kwa wakazi wa kijiji hicho na kuhoji Jamii juu ya muelekeo wa jamii ya Watanzania walioamua kuibomoa wenyewe mila na desturi zetu. 
Bini Condorada Ngonyani anayedaiwa Kufunga Ndoa na Mwanae wa Kumzaa
 Kwa upande wa motto Joseph Mapunda anasema kuwa upendo na mahaba anaopata kutoka kwa mkewe (Mama Mzazi) hajawahi kuyapata kokote na kusema kuwa wanapendana sana na wanaheshimiana kama mke na mume. Josepha amehoji kulikoni watu kuwafuatilia katika mapenzi yao na kusema kuwa ''hawa watu wanaotufuatilia hadi leo hii na kutuweka hadharani namna hii, wanataka nini kwetu?''.
Bwana Joseph Mapunda anayedaiwa kumuoa mama yake Mzazi
Wananchi hao waliofurika kwa Mganga wa Jadi Flora Ndembo wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma, wameiomba Serikali kuingilia kati suala hilo na kuchukua hatua kisheria ili iwe fundisho kwa wanatanzani wengine wenye akili kama hizo za kuharibu mila na desturi za kitanzania kirahisi kama hivyo.

No comments:

Post a Comment