ANGETILE ASIAH - MALAFYALE |
Na mwandishi
wetu:
USAJILI
wa wachezaji kwa klabu za Ligi Kuu Bara, unafikia tamati leo, huku baadhi ya
majina ya yakitarajiwa kuonekana zaidi ya timu moja. Kwa mujibu wa kalenda ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kipindi hicho cha usajili kinachofikia leo
kilianza kwanza Juni 15 mwaka huu. Hata
hivyo, kuna kila dalili ya mgongano wa majina ya wachezaji kwenye usajili huo
kutokana na baadhi ya timu kutoafikiana katika suala la uhamisho wa wachezaji. Wachezaji
wanaoweza kuwa kiini cha mgongano huo, ni mlinzi wa kati, Kelvin Yondani ambaye
Yanga wamesajili kutoka Simba na tayari ameanza kucheza.
Katibu
Mkuu wa TFF, Angetile Osiah Simba wanadai Yondani ni mali yao kwa mujibu wa
mkataba walioingia naye, jambo ambalo limepingwa na mchezaji mwenyewe na hata
klabu yake mpya.
TFF
ilimwihidhinisha Yondani kuichezea Yanga kwenye michuano ya Kombe la Kagame kwa
kile ilichosema, Yanga ilikuwa sahihi kumsajili baada ya mkataba wake na Simba
kumalizika. Lakini
kwa upande Simba, wanadai ni mchezaji wao halali, na watakuwa tayari kwenda
mbele zaidi kisheria iwapo TFF atahidhinishwa kuichezea Yanga kwenye michuano
ya ligi. Katika
hali hiyo, kuna uwezekano mkubwa kwa jina la Yondani kuonekana kwenye orodha ya
Simba, kadhalika na Yanga. Hali iko hivyo kwa Ramadhan Chombo 'Redondo', ambaye Simba wamemsajili kutoka
klabu ya Azam ya Dar es Salaam.
Azam
inasema Simba haikuwa sahihi kumsajili Redondo kwa vile bado ana mkataba halali
na klabu hiyo, jambo ambalo limepingwa na mchezaji mwenyewe. Katikati ya wiki
hii, Redondo alisema mkataba wake na Azam ulishamalizika na hakuwahi kupewa
mwingine, hivyo alikuwa huru kusajiliwa, siyo tu na Simba bali timu nyingine
yoyote.
Pia kuna taarifa, beki wa timu ya APR ya Rwanda, Mbuyi Twite ambaye Simba wanadai wamemalizana naye kwa ajili ya msimu ujao, pia Yanga wamemtengenezea mkakati wa ili kumsajili. Simba wanadai kumpa beki huyo mkataba wa miaka miwili, lakini habari zingine zinadai kuwa Yanga wamefunga safari kumfuata kwa lengo la kufanya naye mazungumzo. Kama kweli, Simba wamemalizina naye beki huyo na taarifa za Yanga za kumtaka na kuingia naye mkataba zikawa za kweli, basi ni wazi kuleta mkanganyiko.
Jumatano
wiki hii, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema iwapo kutatokea suala la
majina ya wachezaji kuonekana zaidi ya timu moja, Kamati ya Maadili, Sheria na
Hadhi za Wachezaji itaamu. Angetile alisema, kanuni za usajili ziko wazi na
klabu zote zinafahamu hilo, hivyo hategemei kuwapo na malumbano kwa vile kanuni
ndizo zitakazopewa nafasi ya kuamua. Kamati
ya TFF inatarajia kupitia majina ya wachezaji yaliyowasilishwa na klabu hizo na
utangaza kipindi cha pingamizi Agost 11 mpaka 18 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment