BM BARBERSHOP KINONDONI

Friday, August 10, 2012

INAONEKANA NI MWEPESI WA KULA KIAPO NA MWEPESI WA KUASI VIAPO


REV: WILBROAD SILAA
 Tujikumbushe kidogo miaka kadhaa iliyopita juu ya Padri Wilbroad Silaa Mtumishi wa Bwana aliyeula kiapo kwa kulala KIFUDIFIDI mbele ya altale Takatifu ya Bwana. Sitaki kukumbuka zamani jinsi mtumishi huyu alivyoapa Kanisani yaani na kuahidi kutomwacha yesu katika maisha yake. Akaapa tena kutomuacha Mke wake hadi kifo kiwatenganishe. Aliapa kuwatumikia wananchi wa Karatu waliompigia kura na kuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwa miaka maka mitano. Juzi alikusudia kuapa tena kuishi na Bibi Josephine kwenye ndoa takatifu. Na sasa anania ya kuapa kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Swali kwanini ulikana viapo vyako vyote hivi??? Tena kubwa zaidi ukakana kiapo chako cha kanisani??? Moto wa milele ukuangazie.aliapa kuilinda na kuitetea imani ya Kanisa Katoliki mbele ya baba Askofu akaapa kua mtii wa kuishika biblia na neno la Mungu kwa upole na unyenyekevu, akakubali kuvaa tenite jeusi. Miaka michache mbele akaasi kiapo cha Mungu je kiapo cha kuilinda Katiba ya Jamuhuri atakitii?? Atakua mtii wa binadamu kama hakumheshimu Mungu?? Kaa chini tafakari chukua hatua mkatae Padre Slaa na mambo yake yoote sio mtu wa kumwamini hata kidogo. NI MTAZAMO WANGU TU.

No comments:

Post a Comment