Waandishi
Wetu
MALAWI
imesema imeondoa ndege zake zilizokuwa zikifanya utafiti wa mafuta katika Ziwa
Nyasa kwa kuwa haitaki kuingia vitani, badala yake imeamua kupeleka mgogoro huo
Mahakama ya Kimataifa. Kauli hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa Mambo ya Ndani na
Uhusiano wa Kimataifa kwa Mambo ya Kiusalama wa Malawi, Uladi Mussa alipokuwa
akizungumza na gazeti linalochapishwa nchini humo la Nyasa Times. “Nawahakikishia
wananchi mtaendelea kuishi kwa utulivu. Tupo kwenye mazungumzo na Serikali ya
Tanzania, bila shaka mambo yataenda vizuri. Kama hali ikishindikana
tutalipeleka suala hili kwenye Mahakama ya Haki ya Kimataifa,” alisema Mussa.
Kauli
ya Waziri huyo imekuja wakati baadhi ya wananchi wa Malawi wanaoishi katika
Vijiji vya Karonga na Chitipa vilivyopo kando ya Ziwa Nyasa upande wa Malawi
wakiwa wameanza kuvihama vijiji hivyo kuhofia usalama wa maisha yao.
Baadhi
ya wakazi hao wamekaririwa na Nyasa Times wakisema kuwa wameamua kuchukua hatua
hiyo kunusuru maisha kutokana na kuwapo kwa dalili za kutokea vita kati ya
Malawi na Tanzania. Waziri Mussa amesema suala hilo la mgogoro wa mpaka
litaamuliwa kwa njia ya amani na hivyo kuwataka wananchi kuendelea na shughuli
zao bila wasiwasi.
Waziri
huyo aliwahakikishia wananchi hao kuwa Serikali ya Malawi ina ushahidi wa
kutosha kuwa ziwa lote la Malawi (Nyasa) ni mali ya Malawi na Tanzania haina
nguvu ya kuwasimamisha kuendelea na kazi ya kutafuta mafuta.
“Kimsingi hapa hakuna hoja ya kubishania. Wote tunajua ziwa hili ni mali yetu (Malawi),” alisema. “Kama malalamiko haya yangekuwa yametolewa na Msumbiji, hapa tungekuwa na hoja ya kubishania, lakini si Tanzania.” alisisitiza.
“Kimsingi hapa hakuna hoja ya kubishania. Wote tunajua ziwa hili ni mali yetu (Malawi),” alisema. “Kama malalamiko haya yangekuwa yametolewa na Msumbiji, hapa tungekuwa na hoja ya kubishania, lakini si Tanzania.” alisisitiza.
Alisema
ushahidi wao wa mipaka ni wa tangu mwaka 1890 wakati ambako wakoloni wa
Uingereza na Ujerumani walitiliana saini juu ya suala hilo. Aliendelea kueleza
kuwa umiliki huo wa ziwa umeongezewa nguvu na maazimio ya mwaka 1963 ya
Wakuu wa uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika (OAU) kwamba wanachama
wanapaswa kuheshimu mipaka waliyorithi kwa wakoloni.
Kauli
za wananchi
Wakati
Serikali ya Malawi ikitoa msimamo huo watu kadhaa waliohojiwa wameonyesha hofu
ya nchi hizo kuingia katika vita. Heckley Christopher ambaye ni raia wa Malawi
anayefanya biashara eneo la Mbambabay mkoani Ruvuma anasema: " Malawi ni
nchi ndogo sana kupigana na Tanzania, ni nchi yenye mikoa minne tu, kukiwa na
vita itaangamia mara moja." Raia mwingine wa Malawi ni Vilion Gordon
ambaye alisema Tanzania na Malawi ni marafiki wa siku nyingi, hivyo hawana
sababu za kugombania ziwa ambalo lilikuwapo tangu enzi hizo. "Nashauri
wakae chini wapatane, kwa nini tugombane sasa wakati ziwa hilo lilikuwapo tangu
enzi hizo?"alisema. Mtanzania mkazi wa Kijiji Lundo kilichoko Mbambabay
mkoani Ruvuma, Zakhia Chengula ameitaka Serikali ya Tanzania kuendelea
kuimarisha ulinzi na kukubali kuingia katika mazungumzo na Malawi badala ya
kufikiri vita.
"Hapa sisi ni kwetu, vita ikiingia sisi tutakufa tu hakuna pa kukimbilia. Tunaiomba Serikali iimarishe ulinzi eneo hilo na ikae na Malawi kuzungumzia mgogoro huo," alisema.
"Hapa sisi ni kwetu, vita ikiingia sisi tutakufa tu hakuna pa kukimbilia. Tunaiomba Serikali iimarishe ulinzi eneo hilo na ikae na Malawi kuzungumzia mgogoro huo," alisema.
Mkuu
wa Wilaya mpya ya Nyasa, Ernest Kahindi alisema hakuna hofu yoyote kwa wakazi
wanaoishi kando ya Ziwa Nyasa upande wa Tanzania. Amewataka wananchi hao
kuendelea na shughuli zao za uzalishaji mali kama kawaida kwani suala hilo sasa
linashughukiliwa kitaifa.
"Mwanzoni kulikuwa na hofu kubwa, lakini
baada ya Serikali ya Tanzania kutoa tamko la kutaka ndege za Malawi ziondoke na
zenyewe kutii amri hiyo, hakuna tatizo lolote," alisema na kuendelea; "Shughuli
katika eneo hili zinaendelea kama kawaida. hakuna mwananchi aliyepigwa risasi
wala ndege iliyotunguliwa, mambo yako shwari." Jeshi laimarisha ulinzi Katika hatua nyingine Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limeimarisha ulinzi katika mwambao wa Ziwa Nyasa na kupiga marufuku wananchi kukatisha eneo lao la jeshi.
Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Kyela waliozungumza na gazeti hili jana walisema kuibuka kwa mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi, kumesababisha kuongezeka kwa ulinzi katika eneo hilo.“Mara ya kwanza tulikuwa tunaingia tu pale kambini kama tumeagizwa vitu kama mayai, vocha na vitu vingine na wanajeshi wa pale tunawapelekea, lakini sasa tangu kuibuka kwa mgogoro huo wa mpaka wa Ziwa Nyasa na hawa wa Malawi tumezuiliwa kabisa kuingia hapa”alisema mkazi mmoja aliyejitambulisha kwa jina Hamis
Chanzo cha hofu Jumatatu wiki hii, akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe aliitaka Malawi kuziondoa ndege na kampuni zinazofanya utafiti wa mafuta katika eneo hilo kwa kuwa ni mali ya Tanzania.
“Serikali ya Tanzania inapenda kuyaonya na kuyataka makampuni yote yanayoendelea na shughuli za utafiti eneo hilo zisitishe mara moja kuanzia leo (Jumatatu),” alisisitiza Membe.
Mbali na Waziri Membe viongozi wengine waliozungumzia mgogoro huo na kuitaka Malawi iache uchokozi ni Samuel Sitta na Mwenyeti wa Kamati ya Bunge ya masuala ya ulinzi, Edward Lowassa. Wakati Sitta akiwataka Watanzania kuendelea nashughuli zao bila hofu kwa kuwa Serikali iko tayari kwa tishio lolote, Lowassa alisisitiza kuwaTanzania imejiandaa kiakili na kivifaa kuingia vitani na Malawi kama italazimika kufanya hivyo.
Habari hii imetayarishwa na Joyce Joliga, Nyasa, Godfrey Kahango, Kyela, Leon Bahati na Mashirika ya Habari
No comments:
Post a Comment