BM BARBERSHOP KINONDONI

Thursday, August 9, 2012

MASHUJAA MUSICA WAREJEA ZIARANI KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI




BENDI ya muziki wa dansi Mashujaa Wana kibega wiki hii walifanya ziara ya maalum katika mikoa ya Mbeya na Ruvuma kwa ajili ya kutambulisha wanamuzi wao wapya pamoja na nyimbo yao ya RISASI KIDOLE utunzi wake Charles Gabriel Mbwana almaalufu Chazbaba Toress.

Akizungumza Dar es Salaam jana usiku na Deo Mutta Mwanatanga muandaaji na Mhariri Mkuu wa Blog ya mwanatanga.blogspot.com Meneja wa bendi hiyo Martin
Sospeter (TAIRO), alisema kuwa wanamuziki wa bendi wataondoka waliondoka siku ya kesho Alhamis kuelekea Songea mjini Mkoani Ruvuma na kufanya onyesho lililofana na kukonga nyoyo za mashabiki wa mji wa Songea katika mwezi huu wa Ramadhani. Meneja Sospeter alisema onyesho la kwanza lilitafanyika kwenye Ukumbi wa Serengeti  Club  uliopo mjini Songea siku ya Ijumaa na baadaye siku ya Jumamosi kwenye ukumbi wa Live uliopo Mbeya Mjini na siku ya Jumapili walimalizia onyesho lao kwa bonanza maalum lililofanyika kwenye ukumbi wa Mbeya City Pub Mbeya mjini.
Meneja Martin Sospeter aliongeza kuwa katika ziara hiyo ambalo lengo lake lilikuwa ni kutambulisha  safu mpya ya bendi hiyo na mtindo wao mpya wa Kibega mambo yalikwenda kama walivyokusudia. Bbendi hiyo imerejea Dar es Salaam jana Jumatano na 
itaendelea na ratiba zake kama kawaida katika kwa ajili ya kuwakonga mashabiki wao kwenye kumbi tofauti za jijini Dar es Salaam kadri watakavyoona inafaa.
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa bendi hii hivi karibuni ilifanya mabadiliko makubwa kwa kuchukuwa wanamuziki wapya ambao ni Charles Gabriel 'Chalz Baba', Soud Mohamed MCD' na Lilian Tungaraza Lilian Internet wote kutoka The African Stars Twanga Pepeta.
Wengine ni Saulo John kutoka katika bendi ya Extra Bongo na Ali Akida mwanamuziki huru. Pamoja na Meneja Martin kutoka Twanga Pepeta ambao wote kwa pamoja wamedai kuwa wameenda kwasababu ya Maslahi. Swali linakuja je maslahi yatakapofikia ukingoni nini kitafuata????





No comments:

Post a Comment