Bibi Banda aliapishwa
kuwa Rais Jumaamosi baada ya kifo cha Rais Bingu wa Mutharika wiki liyopita. Amekuwa
makamu wa Rais tangu mwaka 2009, lakini alikorofishana na Bw Mutharika na
kujiondoa kutoka chama chake kinachotawala. Hakuna sababu iliyotolewa ya
kuondolewa kwa Bw Mukhito, lakini mwandishi wa BBC nchini humo anasema
ameshtumiwa kwa uongozi mbaya wakati wa ghasia za kuipinga serikali zilizotokea
mwaka jana. Bw Mutharika, mwenye umri wa miaka 78, alipatwa na mshtuko wa moyo
siku ya Alhamisi iliyopita ingawa kifo chake hakikuthibitishwa mpaka siku ya
Jumamosi. Alitawala Malawi kwa kipindi cha miaka minane lakini hivi karibuni
alishtumiwa kwa kufisidi uchumi na kutawala kwa mabavu.
Malawi imekumbwa na
ukosefu wa mafuta na fedha za kigeni tangu Uingereza na wahisani wengine kufuta
misaada yao. Mwandishi wa BBC Raphael Tenthani akiwa mjini Blantyre anasema
aliyekuwa mkuu wa polisi alianza kupata sifa mbaya mwaka uliopita baada ya
kumhoji mhadhiri mmoja kwa kulinganisha vuguvugu la upinzani katika nchi za
Tunisia na Misri kuwa sawasawa na mgogoro wa mafuta nchini Malawi. Tukio hilo
hatimaye lilisababisha kufungwa kwa tawi moja la chuo kikuu cha Malawi. Mnamo
mwezi wa Julai mwaka jana ,takriban watu 19 waliuawa kwa kupigwa risasi na
polisi wakati wa maandamano ya kuipinga serikali kuhusu uchumi unaozidi
kuzorota nchini humo. Wakati huo huo maafisa wa serikali wanasema matayarisho
yanafanywa kurudisha maiti ya Rais Muthariika kutoka Afrika ya Kusini ambako
alisafirishwa baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo.
No comments:
Post a Comment