Watu
12 wanaodhaniwa kuwa raia wa nchini Kenya wamefariki dunia papo
hapo na wengine 25 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha
magari manne, ambayo imetokea katika kijiji cha Makole Kata ya Mandera, Tarafa ya Miono Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani wakiwa safarini kuelekea jijini Dar es salam kwenye
shughuli za uimbaji wa kwaya.
Ajali
hiyo iliyotokea majira ya saa 11 alfajiri ilihusisha magari mawili tofauti,
likiwemo lori lililosababisha kufunga kwa barabara na kusababisha abiria waendao katika
maeneo ya kanda ya Kaskazini kuweka kambi katika eneo hilo kwa masaa nane. Kamanda
wa Polisi mkoa wa Pwani Ernest Mangu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na
kusema kuwa gari lenye namba za usajili KBQ 203 P aina ya Isuzu bus, pamoja na
gari lenye namba za usajili KBL 044 M, yote yakitokea nchini Kenya yakiwa
yamebeba waumini wa dini ya kikristo. Ajali
hiyo ni kati ya saba zilizotokea kwa usiku mmoja mkoani Pwani katika barabara
ya Chalinze –Morogoro na Chalinze –Segera.
No comments:
Post a Comment