www.shaffihdauda.com Thursday, August 2, 2012
HIVI NDIVYO ADEN RAGE ALIVYOWAPIGA BAO YANGA NA KUMSAINI MBUYI TWITE
Wakati makamu mwenyekiti
wa Simba Geodfrey Nyange Kaburu na mwenyekiti wa kamati ya usajili Zakaria Hans
Pope wakiwa wanamalizana na kiungo mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa na
mabingwa wa Tanzania bara, upande mwingine mwenyekiti wa klabu hiyo Mheshimiwa
Aden Rage nae alisafiri umbali wa kilomita zipatazo 1,459.7, kutoka Dar kwenda
Kigali kukamilisha usajili wa beki wa kati wa APR Mbuyi Twite.
Wakati Rage akiwa
anamsainisha Twite ambaye pia alikuwa akiwindwa na mabingwa wa Africa mashariki
na kati Yanga - upande mwingine Ngassa alikuwa anatia saini kuitumikia Simba
kwa miaka 2.
Kwa maana hiyo Simba
wakawa wameipiga bao wapinzani wao Yanga ambao wao pia walikuwa wakiwahitaji
wachezaji hao wote wawili Twite na Ngassa.
Na haya ndio matambo ya Simba kupitia msemaji wao
Ezekiel Kamwaga kuhusu kuwapiga bao wapinzani wao.
No comments:
Post a Comment