BENDI
ya Muziki wa Dansi ya Extra Bongo leo imefuturu pamoja na Kituo cha Watoto
Yatima cha Home New Life kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam .
Akizungumza
na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Chocky amesema
wamefanya hivyo ili kuonyesha upendo kwa watoto hao ambao pengine kwa kipindi
kama hiki wangekuwa na Wazazi wao lakini kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu wako
katika mazingira hayo na si kwa ridhaa yao.
Alisema
Chocky wao kama sehemu ya jamii inayowazunguka watoto hao hawanabudi kufanya
hivyo angalau hata Watoto hao nao wajitambue kuwa kana jamii inawazunguka na
inatambua uwepo wao. Chocky alisema kwa mfano huo anawaomba hata Bendi zingine
waige mfano huo na si bendi tu bali hata watu binafsi kwani Watoto hao ni wetu
sote hatuna budi kuwafariji na kufurahi pamoja nao tupatapo nafasi.
Mkurugenzi
wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Choki wakiwa na Mkurugenzi wa kituo cha Kulele
Watoto Yatima cha New Life
Na
Michael Machellah
|
wimbaji wa Bendi ya Extra Bongo, Rama
Pentagon akigawa maadazi kwa watoto wakati wa futari hiyo
No comments:
Post a Comment