![]() |
RAIS WA BENDI YA MASHUJAA CHARLES BABA "TORESS" |
BAADA
ya kukamilisha ziara ya kutambulisha wanamuziki wake wapya wa Mashujaa Band,
sasa ni zamu ya kuwapa burudani wapenzi wa bendi hiyo kwa siku ya Idd Mosi na
Idd Pili.
Meneja
wa Bendi hiyo Martin Sospeter alisema kuwa, siku ya Idd mosi watakuwa Msasani
kwenye ukumbi wa Emirates. Sospeter alisema kuwa, siku ya Idd pili watakuwa
Mjini Mtwara katika ukumbi wa Makonde Beach ili kuwapa radha wakazi wa huko.
Bendi
hiyo ambayo hivi sasa ipo hivi chini ya Rais wake Chalz Baba, itatoa burudani
hiyo kwa ajili ya kutangaza kazi zao mpya kwa wapenzi wa nyimbo zao na Bendi
yao kwa ujumla. Alisema, pia kwa wale wanaoisikia Bendi ya Mashujaa kwenye
vyombo vya Habari, sasa ndiyo wakati wao wa kuiona bendi hiyo laivu katika
Sherehe za Eid El Fitri. “Kama tulivyowapagawisha wakazi wa Songea na Mbeya
wiki iliyopita, sasa ni zamu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na Mtwara,”
alisema Sospeter.
Hahahahaa! walipigia meza viti na kaunta... habari na picha tunazo sisi wa songea
ReplyDelete