BM BARBERSHOP KINONDONI

Monday, August 20, 2012

FASHA AENDA UMANGANI MIEZI MITATU KWA BARAKA ZA ASET

Katika kuonyesha kuwa inajali maisha na maendeleo ya Wasanii Management ya ASET imemruhusu mcheza Shoo wake mahili FASHA kwenda Umangani kufuatia mualiko wa kupata Mkataba wa Miezi Mitatu Uarabuni. Akiongea na mwanatanga mcheza shoo huyo amesema mimi nitafia Twanga kwakuwa kila mara napewa Ruhusa ya kwenda Uarabuni kuhudumu mkataba pindi inapopatikana nafasi. Nawaasa wenzangu waendeleze Makamuzi kwakuwa najua miezi mitatu ni KIDUCHU sana na nitarejea Twanga kuendelea na kazi yangu kama kawaida.

Mcheza shoo huyu aliondoka jana asubuhi kuelekea Umangani na anatarajia kurejea mwezi wa kumi na moja na kuendelea kuitumikia Bendi yake ya Twanga Pepeta iliyompa baraka zote za kwenda Umangani.

No comments:

Post a Comment