BM BARBERSHOP KINONDONI

Friday, August 17, 2012

FERDINAND ATOZWA FAINI KWA LUGHA YA KIBAGUZI.

Beki wa Manchester United Rio Ferdinand ametozwa faini ya pauni za Uingereza 45,000 sawa na dola za kimarekani $71,000 na chama cha mpira cha England baada ya kupatikana na hatia ya kutumia lugha mbovu kwa beki wa Chelsea Ashley Cole.
Halmashauri huru imempata na hatia kwa kumkashifu Cole akitumia lugha inayopdhalilisha ukoo na kabila la mpinzani kwa msemo wa maneno 'Choc ice' kwa maana mtu mweusi nje na ndani mzungu.Ferdinand alikanusha kua sivyo hivyo ila ni kwamba maanake ni mtu feki, au mnafiki. Ashley Cole.Matamshi yaliyopeperushwa kwa mtandao wa Twitter yalitokea baada ya Ashley Cole kutoa ushahidi mahakamani dhidi ya mdogo wake Rio aliyedai kua alitukanwa na John Terry. Terry hakupatikana na hatia.

No comments:

Post a Comment