STALING WA PICHA HII INAYOBAMBA MBUYI TWITE |
YANGA imeifanyia
umafia mkubwa Simba baada ya kumteka na kumsainisha beki Mnyarwanda mzaliwa wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mbuyu Twite ambaye Mwenyekiti wa Wekundu hao,
Ismail Aden Rage alimsainisha pia mjini Kigali wiki iliyopita ili atue
Msimbazi. Mbuyu ni miongoni mwa wachezaji wapya wa Simba waliotajwa kwenye
tamasha la Simba Day, Jumatano iliyopita ingawa hakuwepo nchini. Mashabiki wa
Simba waliofurika kwenye Uwanja wa Taifa walionyeshwa jezi namba 4 ambayo Mbuyu
atakuwa akivaa akiwa Simba. Wapenzi wa Simba walishangilia wakijua kwamba
tatizo limekwisha kwenye safu ya ulinzi kwani Mbuyu atasimama na Juma Nyosso,
lakini sasa hali imebadilika.
Simba ilimpa
mchezaji huyo dola 30,000 (Sh 45 milioni) na kumalizana naye kwa vita iliyodumu
zaidi ya saa nane jijini Kigali, Rwanda ambayo ilipewa jina la Eight Hours in
Kigali, ingawa sasa filamu hiyo imeingia katika sehemu ya pili ukipenda unaweza
kusema Eight Hours in Kigali-2.
Baada ya Yanga
kuchakazwa katika sehemu ya kwanza ya filamu hiyo, waliendelea kupambana vita
ya msituni kupitia kwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Abdallaa Binkleb
na kufanikiwa kumshawishi mchezaji huyo ili arudishe fedha Simba na apewe
kitita kikubwa zaidi.
Mbuyu aliwapigia
simu viongozi wa Simba jana Ijumaa asubuhi akiwaambia kuwa amemtuma mtu
arudishe fedha zao kwani anataka kurudi kuichezea timu yake ya zamani ya Lupopo
ya Congo. Hata hivyo ilivyofika mchana ilikwishafahamika kuwa ameshaini Yanga
kwa kitita kikubwa zaidi. Inadaiwa kuwa amesaini Yanga kwa kitita cha dola
50,000 (Sh 75 milioni)Kisasi Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga na kigogo wa
kamati ya usajili Abdallah Binkleb wiki hii alisema kwamba lazima alipize
kisasi kutokana na nyodo za Simba iliyotangaza kumsainisha Mbuyu Twite kwa
kumgaragaza yeye katika vita ya saa nane mjini Kigali.
Binkleb alitamka
kuwa; "Simba wanasema mimi ni bwana mdogo siwawezi kwa fitna na ujuzi wa
mambo ya mpira, wanasema sina uzoefu wowote kwenye mambo ya mpira, sasa
ninachosema ni kwamba huyo Rage nimemsoma na lazima nilipize kisasi, siwezi
kuvumilia maneno yao. Wanaongea sana mpaka vitu vingine ambavyo havipo
kabisa,"alisisitiza Binkleb na kudai kuwa yupo Kampala lakini ilikuwa
sikweli na liligundua baadaye kwamba alikuwa amejificha Kigali akipanga
mikakati mpaka jana Ijumaa alipomaliza mambo.
Kabange Twite aliulizwa
pacha wa Mbuyu, Kabange baada ya kumkosa Mbuyu na akasema: "Nipo Kinshasa
nafanya mambo yangu lakini nimeongea na Mbuyu aliniambia anakuja kucheza
Tanzania, sijajua kama ni Simba au Yanga, nikiongea naye baadaye ndio
atanihakikishia. "Lakini mimi sina tatizo popote atakapoamua kucheza iwe
Simba au Yanga ni sawa, hizo timu zote ni kubwa na zina mafaranga (fedha)
nyingi, yeye anaenda kutafuta na mimi nitaenda kutafuta, si lazima tucheze timu
moja kama siku zote,"alisema Kabange ambaye amenusurika kwenye rungu la
APR lililopanga kuondoa wachezaji wote ambao si wazaliwa wa Rwanda.
APR imewatema
Logbo Landry Didier (Ivory Coast), Alex De Avila Peixoto, Oliviero Alves na
Douglas Lopes Carneirn (Brazil). FERWAFA Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka la
Rwanda (FERWAFA), Michel Gasingwa amesema kuwa; "Hatuna taarifa yoyote
mpya kuhusiana na huyo mchezaji kujiunga na Simba au Yanga au kuondoka
APR." Kaburu alaani Akizungumzia
hilo, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' alisema
walichokifanya Yanga ni uhuni ambao haukubaliki katika soka. Kaburu alisema
tayari beki huyo alishaini Simba mjini Kigali mbele ya Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage,
viongozi wa Chama cha Soka Rwanda (Ferwafa) na maofisa wa APR. "Tulifanya
makubaliano na Mbuyu wakati wa michuano ya Kombe la Kagame. Tulikubaliana kila
kitu.
Akaomba arudi Rwanda kumalizia mkataba wake na ndipo wiki iliyopita mwenyekiti wangu Rage alipokwenda kumsainisha mkataba wa miaka miwili mjini Kigali mbele ya maofisa wa APR na FERWAFA," alisema Kaburu.
Akaomba arudi Rwanda kumalizia mkataba wake na ndipo wiki iliyopita mwenyekiti wangu Rage alipokwenda kumsainisha mkataba wa miaka miwili mjini Kigali mbele ya maofisa wa APR na FERWAFA," alisema Kaburu.
"Baada ya kusaini aliomba kurudi kwenda kubadilisha pasipoti yake kwao Congo kabla ya kuja Dar es Salaam kuungana na wachezaji wa Simba, lakini tunashangazwa na mambo yanavyoendelea. Tunadhani ametekwa na watu wa Yanga kwa sababu hata simu yake ameibadilisha. Kaburu alisema kuwa walimpa kitita cha dola 30,000 (Sh 45 milioni), lakini Yanga wamempa fedha zaidi. Kaburu alisema kuwa katika jambo la kushangaza Yanga wameomba ITC kupitia Congo, ambako mchezaji huyo amewahi kuchezea klabu ya Lupopo tofauti na kanuni zinavyosema kuwa leseni ya uhamisho wa kimataifa huombwa katika nchi ambako mchezaji amecheza kwa mara ya mwisho yaani Rwanda.
Kaburu alisema
Simba nao haijakaa kimya kwani imeomba ITC kwa Ferwafa na kwamba hawatakuwa
tayari kukubali kushindwa katika hilo. Lupopo Congo Kiongozi mmoja wa Lupopo ya
Congo, ambaye hakutaka jina lake litajwa kwa sababu si msemaji alisema kuwa
Mbuyu ni mchezaji wao na alikuwa amekwenda APR kwa mkopo tu. "Ni kweli
Yanga wamekuja hapa Congo, tumewapatia barua ya kuwaruhusu kumsajili Mbuyu na
tumeipeleka nakala kwa Chama cha Soka Congo. Hivyo Yanga wanaweza kuomba ITC
kupitia chama chetu hapa Congo," alisema kiongozi huyo. Habari ambazo
zilipatikana baadaye zinasema kuwa tayari Yanga walikuwa wamepata uhamisho huo
wa kimataifa kutoka Congo.
No comments:
Post a Comment