Namnukuu Abdallah Bin Kleb
MAMBO matatu yamemfanya beki Mbuyu Twite wa APR ya Rwanda, aachane na Simba SC na kuamua kujiunga na Yanga SC, imebainika baada ya uchunguzi wa kina uliohusisha vyanzo kutoka Tanzania, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Mambo hayo ambayo kwa mjumuisho unaweza kuyaita ‘Ujanja ujanja wa mjini’ wa viongozi wa klabu hiyo ndio leo, yanaiponza klabu hiyo kumpoteza aina ya mchezaji ambaye walimuhitaji sana kwenye kikosi chao ili kujiimarisha.
MOSI; Namna ambavyo ‘walimuenzi’ kiungo Patrick Mutesa Mafisango (sasa marehemu), kwanza klabu hiyo ilivyoutelekeza mwili wa marehemu Mafisango baada ya kifo chake, ambao hakuna kiongozi mkuu wa klabu hjiyo hata mmoja aliyekwenda kumzika DRC, zaidi ya Mjumbe mmoja wa Kamati ya Utendaji na mchezaji mmoja. Pamoja na namna ambavyo Simba hawakujali kabisa mambo mengine muhimu kuhusu marehemu Mafisango, kama arobaini yake na kadhalika, Wakongo wameichukulia hiyo kama ni dharaua na ulipotokea mjadala Mbuyu aende wapi, watu wa Kongo wakamnyooshea kidole kinachoelekeza Jangwani.Ikumbukwe, Mafisango aliyejiunga na Simba akitokea Azam FC, iliyomsajili kutoka APR ya Rwanda, alifariki akiwa mchezaji muhimu ndani ya Simba akiongoza kwa kufunga mabao na mwenye mchango mkubwa kwenye timu.
PILI; Desturi
ya kuwaacha wachezaji wa kigeni baada ya kuwasajili, hata kabla hawajaitumikia
timu mfano Lino Masombo, Derrick Walullya na wengineo na tatu hadhi ya klabu
yao kwa sasa ukilinganisha Yanga na Azam FC.
Habari za kiuchunguzi, ambazo chanzo
imezipata zinasema kwamba Mbuyu alilishwa ‘sumu’ za kutosha ili aichukie Simba,
Simba, hivi karibuni ilimsajili mchezaji Lino Masombo kutoka DRC, lakini baada
ya mwezi mmoja na ushei ikamtema kama ilivyofanya kwa Mganda, Derrick Walullya
msimu uliopita, hilo limetajwa kumsitisha Mbuyu kuangukia Msimbazi na kuamua
kurudisha fedha zote alizochukua kwa Mwenyekiti, Ismail Aden Rage (dola za
kimarekani 30,000 kwa mujibu wa Simba).
TATU: Uwezo
ulioonyeshwa timu ya Yanga hasa Combination ya Mabeki pale nyuma imemkuna sana.
Lino Musombo (Pichani) akifurahi na
Juma Kaseja baada ya kuifunga Azam FC ktk penati kombe la Urafiki.
|
No comments:
Post a Comment