LILIAN INTERNET |
LILIAN TUNGARAZA INTERNET NA ALLY AKIDA TETENAS YA
GENEVA WAIKACHA MASHUJAA MUSICA:
Wanamuziki
wawili waliokuwa Twanga Pepeta kwa miongo mingi walihamia bendi ya Mashujaa
Musica miezi kadhaa iliyopita. Wanamuziki hao ni mnenguaji Lilyan Tungaraza
(Internet) na Mkung'uta gitaa Ally Akida (Tetenas ya Geneva). Meneja wa
Mashujaa Musica wakati huo Maxmillian Luhanga alisema wanamuziki hao
watatambulishwa rasmi katika ukumbi wa Nyumbani Lounge jambo ambalo lilifanyika
kweli. Utambulishio huo ulisindikizwa na Bendi ya Bendi ya Machozi
inayomilikiwa na mwanamuziki Lady Jaydee ambao ndiyo wenyeji wa Nyumbani
Lounge.
Leo
kuna habari zilienea Mitaani na kwenye mitandao ya Kijamii kuwa wanamuziki hao
wako njiani kuikacha bendi hiyo. Kilichoonekana kwenye mitandao hiyo na
mwanatanga kushiriki kwenye mdahalo huo ni kama ifuatavyo:
KUTOKA KUSHOTO NI ADOLPH MBINGA NA ALLY AKIDA TETENAS YA GENEVA |
Karen Filbert Mugishagwe: Kwa hisani ya Shakoor Jongo “Kaka nimeamua kuachana
na bendi ya Mashujaa Musica kwasababu hawana roho ya huruma mimi nilikuwa
namuuguza mwanangu viongozi wote walikuwa na taarifa nashangaa wamenikata kiasi
cha shilingi elfu sitini (60,000) kwenye mshahara wangu si utapeli huu. (HAYO
NI MANENO YA MPIGA GITAA WA BENDI YA MASHUJAA ALLY AKIDA MZEE WA BUNJU)
Samahani lakini kama nitawauzi ndugu zanguni.
KAREN FILBERT MUGISHAGWE... HUYU NDIYE ALIYEANZISHA MADA |
Deo Mutta
Mwanatanga: kaka Shakoor Jongo hebu
tuthibitishie Usemi wa dada Karen Filbert Mugishagwe. Lakini ingekuwa vema kama
ANGETAJA NA MSHAHARA... isije ikawa yeye ndiye kawazulumu Mashujaa Musica......
Alijinadi kwa Mbwembwe pale Channel 5 leo anawaona hawana maana na ni MATAPELI
hivi kuna ukweli hapo???
Mashujaa
Musica: Sisi kazi tu,maneno ya wengine.
Shakor Jongo - Ndugu zangu hasa wapenzi wa burudani ya mziki wa
dansi kuna tetesi nimezisikia kuwa aliyekuwa mnenguaji wa bendi ya Mashujaa
Musica Lilian Internet ameamua kuachana na bendi hiyo huku taarifa zingine
kisema kuwa ameamua kurudi nyumbani. Amesema hawezi kuendelea kuwa
Mashujaa wakati kipindi cha nyuma wakati
anaondoka Twanga pepeta alisema hawezi kuishi na mwanaume asiyezaa (Twanga
Pepeta). Je kama kuna mtu ana husika na ukweli wa tetesi hizi atujuze basi sisi
wana facebook tujue.
SHAKOR JONGO ALITOA MCHANGO MKUBWA WAKATI WA MAJADILIANO YA UVUMI HUU |
Sabiha
Usanga: Uhakika nitakupa kesho ntakapo enda kwake.
Deo Mutta
Mwanatanga: HEEEH kumekucha huko sasa Mara Ally
Akida amekatwa Mshahara mara Internet ... Duuh Panapofuka MOSHI...dada Sabiha Usanga Utujuze ya
Ukweli isije ikawa ya Mbuyi Twite na Simba hahahaha MNALENU JAMBO.... AU Mnawachimba
Mashujaa
Musica..... hapana hizi ni Njama sasa.
Sabiha
Usanga: Deo lazima ntamuuliza na hanifichi kabisa.
Deo Mutta
Mwanatanga: Ninahamu ya kujua Sabiha Usanga ....
Mashujaa
Musica ha ha haaaa
Deo Mutta
Mwanatanga: Tomboka Mashujaa
Musica ili ukomeshe UZUSHI
Mashujaa
Musica: Kuhusu Ally Akida ni kweli hayuko kazini
mwezi sasa,hata ivyo suala lake bado liko ofisini na hajaacha kazi rasmi kwani
ana vitu vya kukabidhi kama ni kweli, Na kuhusu Liliani ni uvumi huo labda
unatokana na yeye kuomba likizo ya Ramadhani huo ni uzushi.
Sabiha
Usanga: Na mimi najua kuwa analikizo kwa ajili ya
ramadhani kwasababu anafunga awezi kuja mazoezini.hayo mengine ndo nayaona hapa.
Deo Mutta
Mwanatanga: This is an Official Statement from Mashujaa Musica..... Who
else will comment on this??? We need the statement From Internet. Hivi Likizo
ni kuacha Kazi??? Haijalishi kama wewe ni Christian kuwa huwezi kuomba Likizo
kwani Lilian Internet ni Muislamu siku hizi Sabiha
Usanga???
Mashujaa
Musica; Ndiyo maana nina uhakika ni uzushi na kuhusu
Ally Akida hajatoa taarifa rasmi hivyo bado ni mfanyakazi mpaka hapo
atakapoandika rasmi barua ya kuacha kwani ana mkataba, hata hivyo tuko tayari
kumuachia kama akitamka rasmi na si kupitia katika magazeti;
Deo Mutta
Mwanatanga; You dont work through News Papers ... GOOD
STRATEGY Mashujaa
Musica... Keep it UP.
Sabiha
Usanga; Na ndo maana mimi nataka kuja twanga
haaaaaaaaaaaaaaa@deo. Kaka Deo haieleweki amesilimu au?@deo.
SABIHA USANGALITOA MCHANGO MKUBWA WAKATI WA MAJADILIANO YA UVUMI HUU |
Mashujaa
Musica: @DEO unajua
strategically ilikuwa lazima uboost jna thru big names lakini trust me ipngo ya
baadae ya bendi ni jina la bendi kwanza na thru the reputed name we can nurture
the young talented...
Shakoor
Jongo: Kuweni wawazi jamani tujue maana jana
nilivyotoka msikitini saa 7 nikapitia kwenye ofisi za Aset na nikamkuta yuko
mazoezini katika kujiandaa na video ya Shamba la Twanga je likizo ya Ramadhani
ni Mashujaa tu ila Twanga anaweza kufanya mazoezi naomba MUONGOZO.
Deo Mutta
Mwanatanga: Huko mtaweza Trust Me Mashujaa Musica You always
know my Strategy.
Deo Mutta
Mwanatanga: Sikujua kaka Respect kama alibadili Dini
unajua kila Mtu anaimani anayoona inaweza kumfikisha kwa Allah/Mungu Respect
kwa maamuzi nya Lili kuwa Muislamu, From Lilian Tungaraza to who sasa. Ila hayo
ni maamuzi Binafsi tumuachie
Mashujaa
Musica: Sasa Shakoor Jongo wewe ni mwandishi na kama
unajua kazi yako,why katika status yako umesema ni habari ziko mtaani kwa nini
hukumalizanma na huyo Liliani ulipomkuta hapo mazoezini? Tubadilike waandishi
tuwe wat wa kureport na kubalance story ushabiki kando na kazii kando,haiwezekani
useme kuna uvumi wakati umemkuta mazoezini why hukupata uhakika?uwazi gani
unaoutaka?ofis ya mashujaa inakuambia yuko likizo.
MASHUJAA MUSICA BAND WALITOA UFAFANUZI KWENYE SAKATA HILI |
Sabiha
Usanga: Kaka Deo sasa Shakoor umemuelewa hapo
anasema amemkuta Lilian mazoezini Twanga Pepeta ya kweli hayo au unamsolola
mashujaa@deo.
Deo Mutta
Mwanatanga: Hee Shakoor Jongo siwezi
kuamini kama Internet anaweza kukanyaga ASET kwa jinsi alivyoapa na
Kukashifiana na Asha Baraka. Acha kutuongopea bwana mimi sijafika ASET kitambo
lakini siwezi kuamini kama Mwanadada huyu anaweza kukanyaga kiwanja kile cha
ASET. Kama ni kweli basi isije ikawa HISTORIA kujirudia ya Choky, Muumini,
Banza na wengine wengi na ikatafsiri ule usemi wa UKIONA PANAFUKA MOSHI.
Naogopa sana kaka. Mimi ninachojua ni kwamba Baby Tall na Sabrina Wamerejea
kutoka umangani na walifika Ofisini kwangu kuniambia Kaka Deo Tumerejea.
Baadaye alikuija Super K Singasinga akanambia kaka nimerejea ila kuna watu
wanataka wanipe Mpunga unanishauri nini??? Nikamuambia mdogo wangu kama Mpunga
uko vizuri Vuta katafute maisha sasa hivi Strategy za Twanga
Pepeta ni Ladies First. Juzi tena kaja Sharapova na Mnenguaji
Bechamp aliyekuwa Acudo baada ya kurejea kutoka Umangani anasema hataki kurudi
Acudo nikamshauri nikamuambia Karibu Twanga hakuna neno. Naipanga safu ya wale
kina dada inanipa matumaini kuwa Ramadhani ikiisha patachimbika. Asha
Sharapova, Baby Tall, Bechamp, Mary Kimwana, Maria Soloma, Vick, Sabrina,
Kiduku, Grace na Fasha hawa ndiyo QUEENS OF TWANGA kuna nini tena hapo kama si
AIBU. Marapa J4, Mirinda Nyeusi, Semsekwa. Waimbaji Saccos Kupaza, Dogo
Rama, Uncle Venna, Hajji BSS, Amigo, Muumini, Kimobitel, Luiza, Badi
Bakule, Janeth Isinika na Nanihiiii......... Huku
Safu ya Nyuma chini ya Kibosho, Shakashia, Sele Tumba, Kanuti, Jojoo, Sele
Soro, Kado Bass, Kaposhoo, Victor Nkambi. Nini kimebakia hapo kama si
Balaa.
Husna Iddy
Sajent: Jamani hayo mambo ya kuingia sehem nakutoka
yapo hakuna cha ajabu km mpira tu leo kaseja yupo yanga nabaada ya muda utackia
yupo samba.
Deo Mutta
Mwanatanga: Umeona eee Mama Watoto Husna Iddy Sajent hata Mashaka Amiri, Millo Severine Mlenga Millo
na Engi Muro Mwanamachame
wanajua hii mambo.
Shakor Jongo
- Sasa nakuwa muwazi ni kwamba ishu iliyoko
mtaani inasemekana Lily anamahusiano ya kimapenzi na mmoja wa vigogo wa bendi
ya Mashujaa (jina kapuni) Sasa kuna kundi la wanenguaji ambao walifukuzwa
Mashujaa Musica nwalienda kupeleka umbea kwa mwenye mume hali ikawa tete hivyo
ili kunusuru na amani iendelee kudumu ndiyo maana Lily anataka kuondoka kwenye bendi hiyo ya
Mashujaa na kurejea kwa mwanaume asiyezaa maneno ambayo aliongea alipoondoka
(Twanga Pepeta) SAMAHANINI LAKINI.
Sabiha
Usanga: kaka deo upo hapo
Husna Iddy
Sajent: Duh!hatariiiiiiii
HUSNA IDDI SAJENT ALITOA MCHANGO MZURI KWENYE HOJA HII |
Deo Mutta
Mwanatanga: Heee
hili nalo Neno??? Sabiha Usanga
sasa Shakoor Jongo kaamua
kufunguka moja kwa moja Duuh Mashujaa
Musica hapa napo panaweza kuwa tatizo japo ni Habari ambazo hazina
Source. Duh Husna Iddy
Sajent Mama watoto naogopa//// Mimi huku aku..... Maisha Binafsi wala>>>>
sasa Jongo kakasirika mimi huyooooooooooooo Kulala.
Mashujaa
Musica: ha ha h a haaa yale yaleeeee hizo habari ipo
mtaani siku nyingi,ndio yale yale strategy chafu cha kuvurugana,tunazo mpaka
message za watu fulani za kujaribu kuwavuruga mnashujaa,ila ukweli ni kwmb hizi
habari b shakoor siyo mpya na hazitauza kwanza Lilian hata kabla hajahamia
mashujaa alikuja kulalamika kwamba anasingiziwa hivi kwa kuwa watu fulani wana
wasiwasi kwamba anataka kuhamia mashujaa,akaambiwa tulishazipata kabla wewe
kama unataka kuja kufanya kazi njoo usiyajali ya watu,wakurugenzi wa mashujaa n
i waelewa sana,hivyo hiyo habari haina ukweli.
Deo Mutta
Mwanatanga: Kaka Millo Severine Mlenga Millo
mimi naogopopa
Shakoor
Jongo: Hizi
si za kuandika ndugu yangu ni mjadala tu ila kama nitaona kuna stori ndani yake
na wasomaji wangu watapenda kuifahmu basi hakuna kitu kitakachonizuia kuandika
kwani ndio wajibu wangu wa kilka siku ila nimefurahi kukiri habari za Ally
Akida lakini za Lily mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmm ila ipo siku ukweli utajulikana
na nitawajulisha tu wajameni Ahsante kaka Ally akida nimeona SMS yako sasa hivi
kwa kunipa mwanga kuhusu hatma yako.
Deo Mutta
Mwanatanga: Mwandishi Shakoor Jongo KAZINI.
Mashujaa
Musica: Sasa sijui tushike lipi,mara nimemkuta
mazzoeini nilipotoka msikitini saa 7 mara saa nakuwa muwazi anatembea na kigogo
wa mashujaa,hayo yote yanaelea,funguka tu umalizie,mwandishi wa habari ni mtu
mkubwa sana katika jamii ni mbaya ukiwa tayari una ushabiki kwani kutapelekea
kutobalanc story zako,mfano habari hii hata kama hjandika katika gazeti lakini
una membes zaidi ya 700 ni wengi kuwafikiashia habari kama hii,ebu fuatilia wakurugenzi
wote wa mabendi fuatilia aishayao binafsi utakuta wengine wanatemba nvitoo
vidogo lakini haya hayana maana.
Shakoor
Jongo: Humu si gazetini ni mtandao wa kijamii ila
kama uanataka kuendeleza hoja nimeamia Jamii Forum kuna hoja zingine
zinaendelea njoo huku tuendeleze maana naona unataka kuhakikishiwa mimi siwezi
kuendelea kukaa humu facebook kwani nishaaga muda mrefu SAMHANI LAKINI
Mashujaa
Musica: kKani tofauti ya gazeti na umu ninini?kote
habari zinawafikia watu kaka.acha hizo habri zilizoko mitaani zipo nyingi mbona
zinazowahusu wakurugenzi wote wa mabendi mbona hujazitaja?
Husna Iddy Sajent:
Mie mpk sasa cjaona cha ajabu cz mashujaa ilikuwepo kabla ya lili na inafanya
vzr tu na khsu kuja kwake ikawa poa na walimpokea km mtu mwngne tu alieomba
kazi kwa hy kama kuna chochote ataiambia ofisi kama alivyoenda kuomba kazi sasa
mbona kama imekua big inshu vile mnataka kuifanya,cz ofis@mashujaa musica
ishawajibu amesema anaomba mapumziko ya kufunga mwez km kuna jipya mtajua jaman.
LILIAN TUNGARAZA INTERNET |
Shakor Jongo:
Jamani sasa naenda
kulala huu mjadala tutaendeleza kesho kama kutakuwa na humuimu ila nakuhaidini
kesho nitakuja na hoja mpya ila kama kuna mtu anataka kuendeleza hoja na kujibiwa
haraka sana basi nioneni kwa namba hii 0767 244131 nitawajibu na
ninachokifahamu SAMAHANINI LAKINI Byeeeeeeeeee.
Deo Mutta
Mwanatanga: Mimi nitakupigia kaka... Hata Millo Severine Mlenga Millo
amesema atakupigia.
Shakoor
Jongo: Sawa kaka nasubiri simu yako.
MWANATANGA ALIKUWA MCHOMBEZAJI ILI KUPATA TAARIFA SAHIHI |
No comments:
Post a Comment