NAKUULIZA OKWI!!!! HIVI KWELI ULIENDA ULAYA KWENYE MAJARIBIO AU MAGUMASHI???
NAKUULIZA OKWI!!!! HIVI
KWELI ULIENDA ULAYA KWENYE MAJARIBIO AU MAGUMASHI???
Mambo vipi kwanza!!! Pole
kwa kuugua Malaria ndugu yangu.
Kwa kuwa umepona hebu ngoja niulize…najua wewe hutaweza
kunijibu moja kwa moja lakini wapo watu wako wa karibu wanaweza kukujibia.
Hivi Okwi ..ni kweli uliitwa kufanya majaribio
ulaya???? Maana mwenzako nina mashaka kweli na hili jambo. Na siku ile Kaburu lipokupigia
simu hivi ulikuwa wapi?? Au ndiyo Uganda vile eti!!!!
Ehee!! Okwi sasa kule ulaya timu gani vile hivi ni
Parma au Intermilan. Mwenzako sijui kabisa.
Kweli Okwi yaani safari ndefu kama ile Okwi hukubeba
Camera kwa jinsi waafrika tunavyopenda sifa lazima ulibeba bwana. Okwi wewe si
unajua Kiingereza kabisa, hivi ulipokuwa unafanya mazoezi na hao Parma
ulishindwa kumwomba mchezaji mmoja akupige picha uwatumie Mwanaspoti wauzie
gazeti?? Ka Ngassa kenzako kalikuwa
kajanja kalipiga picha na yule nani yuuule Zola. Eeh!! Zole aliyechezaga
Chelsea. Tukamwona na jezi ya Westham Ngassa na hizo picha zipo hadi leo
mtandaoni.
Akampiga chenga Rio Ferdinand na yenyewe akapigwa
picha akatuma. Sasa vipi wewe Okwi mbona hukufanya hivyo?? Au hupendi sifa
wewe.
Halafu Mwenyekiti wako Aden Rage kwenye mkutano katuambia umefuzu majaribio na
utauzwa Bilioni 11 ambazo zitatumika kujenga uwanja wenu kule Bunju. Mh!!
Hongera Okwi kwa hilo. Tena na milioni sita kwa mwezi mwenzangu umetoka
kimaisha tayari…mi hata ada ya kujiendeleza kimasomo sina.
Lakini kingine cha ajabu nimesikia umeongeza mkataba wa miaka miwili na Simba heee!!
Mwenzangu makubwa hayo. Ina maana kumbe umefuzu halafu baada ya miaka miwili
ndo unaenda kucheza??? Ulaya imebadilika aisee!!!! Yaani wamepanga kukununua
bila kujua kama unaweza kupata majeruhi ndani ya hiyo miaka miwili???
Mh!! Ema rafiki mimi nina mashaka na wewe, siasa
zetu za bongo zimeanza kukutawala na wewe…tena zimekukaa damuni..unadiriki
kutufanyia ulaghai kama huo kweli?? Okwi jamani dah!!! Imeniuma kweli!!!!
Halafu huyo Mwenyekiti wako kweli anajielewa huyo??? Anaongeaongea tu ilimradi.
Mara umefuzu mara umesaini mkataba. Kha!!!! Mwambie anapoteza mvuto katika
jamii.
Kwa leo yangu ni hayo bwana Okwi. Lakini ukienda
siku nyingine ulaya upige picha kama kina Ngassa, Mrwanda, Henry Joseph, Nizar
Khalfani na wengineo.
Maana sisi kuamini mpaka picha. Lakini kama ulipiga kweli naomba uni-TAG
Wako katika michezo, Lady Tina kutoka WAKALI WA TERMINAL, UBUNGO!!!
No comments:
Post a Comment