Mwenyekiti wa klabu ya soka Simba Alhaji
Ismail Aden Rage amesema amesikitishwa na kitendo kilicho fanywa na mahasimu
wao katika soka Yanga kwenda kumsajili mlinzi wa Kati wa klabu ya APR ya Rwanda
Mbuyi Twite kinyume na taratibu za kisoka.
Akiongea na waandishi wa Habari
mjini Dodoma Rage amesema kitendo hicho ni sawa na unyama na si uungwana kwani
tayari walikwishamalizana na mchezaji huyo lakini kitendo kilichofanywa na
Yanga kwa kushirikiana na shirikisho la soka nchini Tanzania TFF si uungwana
kabisa.
Rage amesema wao kama Simba tayari
walimpatia Mbuyi Twite dola elfu 30 kwa mkataba wa miaka miwili na kimsingi
walikubaliana naye mbele ya Rais wa klabu ya APR Meja Jenerali Alex Kagame. Lakini
wakati Simba wakidhani wameshayamaliza na wakiwa wanamsubiri Mbuyi Twitte kutua
Msimbazi ndipo mambo yalipo badilika na taarifa kuifikia Simba kuwa mchezaji
huyo amesajiliwa na wapinzani wao Yanga.
Rage amesema kilichofanywa na Yanga
wakishirikiana na TFF ni kutumia wakubwa na hasa akimtaja mtoto wa Kigogo ambaye
hakuwa tayari kumtaja jina lake ambaye naye aliwatumia wakubwa wa Rwanda
kukamilisha usajili wa Mbuyi Twite ambaye kwasasa anawasubiri Yanga ambao wana
ratiba ya kwenda kuweka akambi nchini Rwanda.
Rage amesema wakati taarifa hizo
zikiwa zimewafikia Simba aliamua kumpigia simu Rais wa APR Meja Jenerali Alex
Kagame ambaye alimthibitishia kuwa ni kweli klabu yake ilitoa ruhusa Simba
kumchukua Mbuyi na si Yanga lakini kilicho fanyika ni kuwa amepewa maagizo na
wakubwa kumsainisha Twite katika klabu ya Yanga na hivyo taratibu za uhamisho
zikafanyika ili mchezaji huyo ajiunge na Yanga.
Rage amesema hilo limemsikitisha
yeye na uongozi wote wa Simba na kuwataka wanachama na wapenzi wa Simba wawe
watulivu kwa mambo hayo yana mwisho. Kwasasa Rage amesema wao kama Simba
wamekubali yaishe isipokuwa wanaomba mchezaji huyo kurudisha pesa alizochukua
baada ya makubaliano na Simba ikiwa ni pamoja na dola elfu 30,000 za usajili
wake, gharama za usafiri wa kwenda Kigali mpaka Lubumbashi na kisha kurejea Dar
es salaam na hoteli, pamoja na gharama za kuwalipa mawakili waliosimamia zoezi
la usajili wake kisheria ambazo kwa ujumla wake ni kiasi wa dolari za
kiamrekani 9,000.
Rage amesema hilo likishindikana
watalazimika kupeleka mashtaka shirikisho la soka duniani FIFA kutokana na
kitendo cha kitapeli kilichofanywa na mchezaji huyo kujisajili vilabu viwili.
IPO SIKU TIMU ZISIZO NA WAKUBWA ZITAPIGIWA KURA YA HURUMA NA JAMII. NALAANI VIKALI KITENDO WALICHOFANYA YANGA NA KUHUSISHA VIONGOZI AU WATOTO WA VIONGOZI WA KISIASA KUHARIBU MIPANGO YA SIMBA. NAWALAANI NA NAWAOMBEA MABAYA BAADA YA BABA ZAO KUACHA UONGOZI WA SIASA --- NA YAWAKUTE MABAYA NA MAAFA KWA LAANA HII NA WATU WAWASAHAU KABISA DUNIANI KWA ROHO MBAYA YA KUKOSA UPENDO NA MSHIKAMANO WA KISOKA. HAKUNA UNAZI WA HIVYO HIYO NI DHULUMA NA KUKOSA UUNGWANA NA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA NA DHAMANA VIGOGO NA FAMILIA ZAO WALIYOPEWA NA WANANCHI.... MWISHO WA KUJINUKUU
ReplyDelete