WADAU WA SOKA TABIA YA ALHAJI RAGE KULIALIA
KILA ANAPOKOSEA NITABIA YAKE YA KUKAMILISHA HADAA ZAKE KUWENI MAKINI.
MOSI: Alhaji Rage alishawahi kulia wakati Mchezaji aliyetoa mchango mkubwa kwenye
timu ya Simba Marehemu Patrick Mutesa Mafisango Papaa alipofariki kwa ajali ya
gari miezi kadhaa iliyopita. Lakini Uongozi wa Rage umeshindwa kuwasilisha pesa
za Rambirambi kwa familia ya Mafisango kama walivyoahidi hadi leo 12/08/2012.
Uongozi wa Alhaji Aden Rage kupitia
Msemaji wa Club ya Simba Ezekiel Kamwaga umesema haujutii kutupwa nje ya nyumba
vyombo vya Marehemu Mafisango.Kamwaga aliongeza kuwa mkataba wa nyumba hiyo
aliyokuwa akiishi mafisango ambao uliingiwa na Club ya Simba ulikuwa ni kwa
ajili ya kuishi mafisango na ulishamalizika tangu mwezi uliopita (30/07/2012)
hivyo mwenyenyumba alikuwa na haki ya kutupa vyomba nje kwakuwa watu wanaoishi
humo hata Simba haiwatambui. Aliyekuwa akiishi
humo ni nduguye Mafisango ambaye alikuwa anasubiri kukabidhiwa rambirambi ili
arejee DRC.
Aidha uongozi wa Simba SC umesema
kuwa, Simba ilikuwa inasubiri Familia iteue Msimamizi wa Mirathi ili akabidhiwe
fedha hizo za rambirambi jambo ambalo baada ya kutekelezwa na familia Uongozi
wa Alhaji ukasema kuwa Ubalozi wa CONGO
nchini Tanzania umeizuia Simba kukabidhi rambirambi hizo kwasasa. Sasa hivi
tena Simba kupitia kwa Katibu wa Simba SC Bwana Evodius Mtawala imekuja na
kauli nyingine kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
umeingilia kati stahili za Mafisango na kuzisimamisha hadi hapo itakapotoa
TAMKO. Hivi Wizara ya Mambo ya Nje kuingilia stahili za marehemu tena raia wa
kawaida tu inaingia akilini???
PILI: Rage alilia
wakati anashitakiwa kwa pesa za Yanga dola 40,000 miaka kadhaa iliyopita na
baadaye kutumikia kifungo na kutoka kwa msamaha wa Raisi.
TATU: Alhaji Rage kwenye Mkutano wa Simba 08/08/2012 takribani siku
sita zilizopita aliwahakikishia Wanachama wa Simba kuwa Okwi amefanya majaribio
na kufuzu katika Klabu ya Red Bull Salzburg ya Australia na atakuwa akilipwa
Euro 300,000 kwa mwezi. Cha ajabu Okwi
amekanusha kufanya majaribio yoyote Ulaya kutokana na kusumbuliwa na Malaria
tangu awasili barani humo mpaka kurejea Uganda na kisha Simba. Alhaji Rage
alipoulizwa kuwa haoni kama aliwadanganya wanachama wa Simba kwakuwa Okwi
amekanusha usemi wake, Rage alisema Okwi hakwenda kutalii amini ninachosema
hicho ni sahihi mimi ni muislam. Kwa mujibu wa mtandao rasmi wa Red Bull
Salzburg ni kwamba timu hiyo imesajili wachezaji wawili tu kati ya tarehe ambazo
Okwi alikuwa Ulaya mpkana anarejea Uganda wachezaji hao ni pamoja na: Valon
Berisha kutoka Viking Stavanger na Havard Nielsen kutoka Valerenga Oslo zote za
Norway.
NNE: Alhaji Rage amelia jana 11/08/2012 Mjini Dodoma mbele ya
waandishi wa habari ili wanasimba wamuamini baada ya kumkosa Mbuyi Twite. Kinyume
na matarajio ya wengi alikurupuka na kudai kuwa pesa waliyotumia Yanga ni pesa
ya EPA. Hii ni tuhuma nzito inayoweza kumghalimu siku za usoni japo ameapa kuwa
haogopi mtu yoyote katika hili.
TANO: Alhaji Rage ameonyesha dhahili kuwashawishi mamilioni ya Wanasimba
kuichukia Serikali ambayo yeye ni mmoja wao (Mheshimiwa Mbunge wa Tabora Mjini)
kuwa wanaonewa na kadai kuwa amepata
ridhaa ya kusema hivyo kutoka kwa wanasimba. Je mkutano wa kudhibitisha kauli
hii umefanyika lini???Kauli inayoonyesha Uchochezi na Uasi hii hapa nanukuu “Kama
Serikali na Mamlaka za kusimamia soka zitaonekana zinapendelea timu moja, basi
wanachama wa Simba wanaweza kuangalia kwingineko ambako wanadhani watapata haki
zao za msingi” KILIO. Alhaji Rage hajatoa ufafanuzi wa kina juu ya kuingia kwa
Serikali katika suala la kuonewa kwa Simba alikodai wala kama amepewa RIDHAA na
wanachama wa Simba kuishutumu Serikali yao kwa niaba yao akiwa Mbunge kupitia
chama kinachotawala. KUENI MAKINI NA MTU HUYU.
No comments:
Post a Comment