TAARIFA RASMI YA YANGA KUHUSU USAJILI WA MBUYI TWITE
Mbuyu Twite (kushoto) akiweka alama ya dole gumba katika mkataba wake mpya wa kuitumikia timu ya Young Africans wiki mbili zilizopita, kulia kwake ni mjumbe wa kamati ya Utendaji Abdallah Bin Kleb |
Mlinzi
wa kati wa timu ya APR kutoka nchini Rwanda Mbuyu Twite amekamilisha usajili
wake ikiwa ni pamoja na kupata uhamisho wa kimataifa ITC na kuweza kujiunga na
mabingwa wa kombe la klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kombe la Kagame timu
ya Young Africans Sports Club. Mbuyu
Twite amabye zoezi lake la usajili lilianza takribani wiki mbili zilizopita
limefikia mwisho baada ya klabu ya Young Africans kufanikiwa kupata uhamisho
wake wa kimataifa kutoka timu aliyokuwa akiichezea ya APR ambapo awali alikuwa
akiichezea timu ya st. Lumpopo FC Mbuyu Twite akiweka saini katika mkataba wake
mpaya na timu ya Young Africans. Twite ambaye alingara sana katika mashindano
ya Kagame yaliyomalizika hivi karibuni na Young Africans kuibuka mabingwa,
amesema anajisikia furaha na mwenye bahati kufanikiwa kujiunga na mabingwa mara
mbili mfululizo wa kombe la Kagame.
Mbuyu Twite akiweka saini katika mkataba wake mpaya na timu ya Young Africans |
Usajili
wa Twite ulianza takribani wiki mbili zilizopita ambapo mjumbe wa kamati ya
Utendaji wa klabu ya Young Africans Abdallah Bin Kleb aliamua kwenda nchini
Rwanda kuhakiksiha zoezi hilo linakamilika haraka ipasavyo, ambapo mara baada
ya kumalizana na Twite aliendelea kuhakikisha anafuatilia ITC yake nchini DRC.Akiongea
na www.youngafricans.co.tz Bin
Kleb amesema, Young Africans ni timu kubwa katika Ukanda huu, Viongozi wake
wanafanya mambo yao kwa uhakika zaidi, hivyo hawakutaka kuongelea suala la
Twite mpaka watakapoona wamekamilisha zoezi lote'
Abdaalh Bin Kleb (kushoto) akimkabidhi jezi mchezaji mpya kutoka APR Mbuyu Twite |
"Unajua
usajili sio mchezaji kusaini makaratasi ya mkataba tu, kuna kupata barua ya
kumruhusu kutoka timu anayotoka, uhamisho wa mchezaji kutoka chama husika cha
soka cha nchi, baada ya hapo ndio unaweza kutangaza sasa kwamba ni mchezaji
wako halali"alisema Bin Kleb.Kusajiliwa kwa Mbuyu Twite kunaifanya timu ya
Young Africans kuwa na ukuta wa walinzi wa kimataifa akiwemo Kelvin Yondani,
Nadir Haroub Cannavaro, Ladislau Mbogo na Ibrahim Job kwa nafasi ya ulinzi wa
katikati. Twite anatarajiwa kuwasili mapema wikii kuungana na wacheji wenzake
katika mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara
inayotarajiwa kuaanza sepetemba mo
No comments:
Post a Comment