BM BARBERSHOP KINONDONI

Sunday, August 12, 2012

SIMBA YATOA MKATABA WA TWITE KUWAKATA NGEBE YANGA

DOSALI SABA KWENYE MKATABA KATI YA MBUYU TWITE NA SIMBA SC KWA MTAZAMO WANGU.
TWITE NA RAGE
Klabu ya Simba SC leo imetoa hadharani mkataba wake uliosaniwa  kati yao na Mchezaji wa kimataifa kutoka Rwanda Mbuyi Twite ambaye jana iliripotiwa kuwa amesaini pia mwingine wa kujiunga na Yanga SC.
huu hapa:









1.      Neno NULL & VOID nadhani huwa lina maana nzito sana japo mimi si mwanasheria, lakini nadhani Simba wanayohaja ya kulitazama kwa mapana yake. Nilivyoelewa na nijuavyo nadhani Simba wamekiuka maana ya maneno haya kwa kushuhudia uongo kuwa mkataba umesainiwa tarehe 01/08/2012 Kigali Rwanda Mbele ya Mwenyekiti wa Simba Alhaji Ismail Aden Rage, Katibu wa Simba Evodius Mtawala na Advocate Frank Philemoni Milanzi wa S.L.P 12800 Dar es Salaam. Kuanzia 01.08.2012-31.07.2014 kwa mshahara dola za kimarekani 2,500. Viongozi wa Simba wanasema walimtuma kwenda Rwanda kukubaliana modality na mchezaji husika pamoja na kuonana na uongozi wa chama cha soka cha Rwanda ili waweze kukubaliana juu ya suala la mchezaji TWITE. Swali langu sasa mbona mkataba kati yao unaonyesha kusainiwa Dar es Salaam na Si Kigali Rwanda??? Suala hili kisheria linaondoa uhalali wa mkataba. Rage alitamka wazi mbele ya waandishi kwa nyakati tofauti kuwa mkataba umetiwa saini Kigali Rwanda wakati kwenye Mkataba inaonyesha kuwa Mkataba umetiwa Sahihi zimetiwa Dar es Salaam.  Je na hii ni HUMAN ERROR tena kama ile ya Kelvin Yondani? Kwa upeo wangu mdogo kisheria kile Kipengele kinachosema  "IMETIWA SAHIHI NA.....HAPA.....LEO TAREHE......." huwa kina maana yake na ndiyo maana hujumuishwa kwenye mikataba yoteNI MTAZAMO TU.

2.      Kipengele namba Saba cha mkataba husika kinasema “Kwamba MCHEZAJI atahesabiwa kuwa Mchezaji Halali wa Simba pale tu usajili wake utakapokubaliwa , kurithiwa na kudhibitishwa na TFF” Swali je haya yalishatimia hadi Simba walalamikie kuwa Yanga wamewachezea Faulu???

3.      Kwenye ukurasa wa kwanza wa Mkataba huu umeonyesha kuwa Simba inaingia Mkataba na MBUYI TWITE wa Kigali Rwanda lakini kwenye ukurasa wa mwisho wa mkataba husika imeonyesha kuwa aliyeingia Mkataba ni MBUYU TWITE na si MBUYI TWITE Yule anayeonekana kwenye ukurasa wa Kwanza. Je na hii ni HUMAN ERROR tena kama ile ya Kelvin Yondani?

4.      Hivi Mchezaji wa Kimataifa (Professional Player)  kumsainisha Mkataba ulioandikwa kwa Kiswahili sidhani kama huyo Mbuyu Twite anajua kiswahili vizuri???

5.      Huwa kuna utaratibu wa kutia Saini kwenye kila Ukurasa (Page) kwa waingia ili kuweka mazingira ya kuepusha Fojali. Kwenye Mkataba inaonekana Sahihi (Siganature) ya Alhaji Rage pekee je ya Twite ilisahaulika wakati mwanasheria aliyesimamia zoezi hili anajua Utaratibu???  Je na hii ni HUMAN ERROR tena kama ile ya Kelvin Yondani?

6.      Mkataba wa Mchezaji kwa nini uwe na sehemu ya cheo chini ya sehemu ya sahihi na jina? Yawezekana CHEO si kosa ila hapa nadhani pia Was Wrong na ndiyo maana Mchezaji hakujaza sehemu hiyo ya CHEO?

7.      Hivi huyu Mchezaji hana Anwani??? Kwakuwa Anwani si lazima iwe Box ya Paosta hata neon Kigali Rwanda au Lubumbashi Congo ingefaa kuonyesha kukubali na kumuelewesha Third Peole pindi kukiwa na utata kuwa Kweli mimi ni mtu wa Rwanda au Congo. Je Mwanasheria hili analisemea Vipi???
Ikumbukwe kuwa ile incidence ya usajili wa Kevin Yondani kuna baadhi ya mambo yalizungumzwa na kuonekana kama ni DOSALI kama vile  "YONDAN" NA "YONDANI" au tofauti ya umri wa miaka "17" na "28".
USHAURI- Mheshimiwa Mbunge, Mwenyekiti wa Simba SC na Alhaji Ismail Aden Rage aache kukejeli watu au KUTUKANA MAMBA KABLA YA KUVUKA MTO. KUMUWEKA MTU Loud Speaker “nipo na bamutu ba samba” ni UDHALILISHAJI umehukumiwa na mambo yako na sasa yanakurudi ACHA KUTAFUTA UTETEZI.

No comments:

Post a Comment