FURAHIA USIKU WA SINA MUDA HUO NA JAHAZI MODERN
TAARAB
Wakazi wa Dar es Salaam na Mikoa ya Jirani ya Pwani, Morogoro
na Tanga baada ya kuikosa burudani waliyoizoe kutoka kwa Bendi isiyo na
Mpinzania kwenye GHANI za Miziki ya MWAMBAO almaarufu TAARAB kutoka kwa JAHAZI
MODERN TAARAB Chini ya MFALME MZEE YUSUF
wameandaa onyesho kubwa na la aina yake siku ya Jumapili 26/8/2012 ndani ya ukumbi wao wa nyumbani, Travertine Hotel
Magomeni.
Onyesho limeandaliwa maalum kabisa na kupewa jina la "USIKU WA SINA MUDA HUO" ambalo
ni onyesho la kwanza kabisa baada ya mfungo wa Ramadhani. Kwa mujibu wa Mzee
Yusuf wakati akiongea na Mwanatanga alisema kuwa nanukuu “Nitashuka na vionjo
vipya kabisa nilivyovifanyia kazi kwa tariban mwezi mzima wakati wa mapumziko
ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Kama ilivyoada mimi naanzisha nawengine wanafuata,
si onyesho la kukosa kabisa, nataka kuudhihirishia ulimwengu kuwa mimi
nimezaliwa kwa ajili ya Taarab.
Kiingilio katika onyesho hilo ni shilingi 8,000/= tu za
Kitanzania, Ukitoa Buku Kumi unarudishiwa chenji inayotosha kupata kinywaji. Si
Onyesho la kukosa…..
MUAMBIE
HUYO, WALE, WEWE, HUYU PAMOJA NA YULEEEE KUWA TRAVETINE HOTEL NI KIVUMBI SIKU
YA JUMAPILI
No comments:
Post a Comment