ISSA HASSAN "COMPUTER" MAPACHA 3 |
Issa Hassan (Computer) ni mpiga Drum ambaye huwezi kumfananisha na
yeyote hapa Bongo kwasasa huo ni ukweli usio na Doa kwa sisi tunaojua Miziki.
Sitakataa wengi wakisema nimekosea lakini ukweli utaniweka huru siku zote.
Issa Hassa alizaliwa 14 March 1987 akiwa ni mtoto wa mwisho kwenye familia ya
Mzee Hassan. Compuetr kama anavyoitwa na mashabiki wake alianza kazi ya Muziki
akiwa darasa la nne Shule ya Msingi Majengo Songea wakati huo akiwa kama DANCER
(Mcheza Shoo) Mimi huwa napenda kuwaita wachezesha Nyonga ambao huwa ni
kinogesho kizuri kwenye masuala ya Miziki. Kazi ya Unenguaji au Ucheza shoo
alidumu nayo kwa miaka nane na baadaye kuanza kujifunza kucharaza DRUM kazi
ambayo hadi sasa ndiyo iliyomjengea jina na kumpatia RIZIKI.
Kazi hii ya kupiga Drum nilikomaa nayo na nikawa makini zaidi na
kujitokeza kwenye jumuiya ya Wapiga Drum pale Morogoro Mji Kasoro Bahari nikiwa
na bendi ya ELEVERT MUSICA bendi ambayo pia ilishawahi kuimbia Mwanamuziki
Baddy Bakule Jogoo la Mjini ambaye sasa yuko na Twanga Pepeta SUGU.
Mwanamuziki Elyston Angai alivutiwa na upigaji wangu wa Drum na
alikitambua Kipaji change na kuamua kunichukua na kuniingiza kwenye Bendi ya
Vibration Sound iliyokuwa chini ya ASET ambayo sasa ndiyo Mashujaa Band.
Nilidumu na bendi ya Vibration hadi ilipochukuliwa na Mama Sakina na kuwa
Mashujaa Band na niliitumikia kwa uadilifu mkubwa na kutoa mchango wangu ambao
nadhani hautasahaulika. Kutokana na umahili huu wa upigaji wa Drum ndugu zangu
wa Mapacha Watatu waliniona na kunifuata kuniomba nifanye nao kazi hadi sasa
ninaitumikia bendi ya Mapacha Watatu kwenye kila Kazi unayoisikia kuanzia Albam
ya Jasho la Mtu hadi leo hii.
Ndoto
zangu za baadaye ni kumiliki bendi yangu na kuwa na studio ambayo itarekodi
kazi za Wasanii hususan wa Kipato cha Chini kwakuwa najua huko chini wapo
watoto wanaojua ambao wanaweza kuwaezi vilivyo kina Marehemu Abuu Semhando na
Gabbi Katanga ambao walikuwa niwapigaji wazuri sana wa Drums.
No comments:
Post a Comment