RAISI JOYCE BANDA WA MALAWI |
Na.
Cedrick Ngalande wa Nyasa Times
Muda mchache
baada ya kupata Uhuru watu wachache kutoka Tanzania walitaka kudai eneo kubwa
la Ziwa Malawi au Ziwa Nyasa kuwa liko upande wa Tanzania. Vichwa makini wakati
huo vya Watanzania akiwemo Rais Julius Nyerere, walielewa umuhimu wa kuheshimu
mipaka iliyowekwa wakati wa utawala wa Kikoloni.
HUYU NI CEDRICK NGALANDE WA NYASA TIMES MUANDISHI WA MAKALA HII KWA KIINGEREZA NA KUTAFSIRIWA KWA KISWAHILI ILI KUSAIDIA WATANZANIA WENGI KUELEWA ALICHOKUSUDIA MUANDISHI HUYU |
Wakati wa
utawala wa Hayati Dr Kamuzu Banda, Tanzania haijawahi kuendeleza mdahalo huu wa
kijinga wa kutaka kuliteka Ziwa Malawi/Nyasa. Suala hili pia halikuweza
kufanyiwa kazi wakati wa Utawala wa Raisi Dr Bakili Muluzi na wote waliofuata
baada yake. Wakati wa utawala wa Dr Bingu wa Mutharika aliamua kuipatia Kampuni
moja kufanya utafiti wa Mafuta kwenye Ziwa hilo. Tanzania haikusema chochote
wakati utafiti huu ulipoanza kufanyika. Wakati huu tukiwa na rais Mpya Mwanamke
ghafla Serikali ya Tanzania wanaitaka Serikali yetu isimamishe shughuli zote za
kitafiti kwenye Ziwa Malawi/Nyasa mpaka suala la mipaka litakapojadiliwa na
kuwekwa vizuri. Kwanini Sasa????
Wananchi, kuna sababu
kwanini Wamalawi tuna Utamaduni. Utamaduni utakuwa hauna maana au unaweza kuwa umepitwa
na wakati lakini ni muhimu kwakuwa ulianzishwa muda mrefu uliopita hivyo uheshimiwe.
Kwenye Siasa kuna kitu kinaitwa ITIFAKI YA RAIS (‘presidential protocol’). Kuna
vitu vidogovidogo ambavyo kwa miaka mingi vimeonyesha kuwa nivizuri na Raisi
anaweza au asiweze kuvifanya ili kuwakilisha nchi yake vizuri na kwa usahihi
kuepuka mizozo isiyo ya lazima.
MTIHANI WA RAIS JOYCE BANDA KUKABILI UTATA HUU WA MPAKA
KIDIPLOMASIA
Unaweza
kudhani kuwa wengine mengine si muhimu lakini ni muhimu sana. Baadhi ya masuala
hayo ni kama ifuatavyo;
- Rais hawezi kuwasema maraisi wenzake vibaya hadharani,
- Raisi hawezi kumsindikiza Rais mwenzake kwenda kwenye gari;
- Marais hutembea na majeshi kama ngao kwa ajili ya kulinda miradi yao ya Kinchi.
- Maraisi huwa na rangi moja isiyoyumba na kubadilika kwakuwa inaonyesha kujiamini.
- Kama Maraisi wawili wakiwa wanasalimiana huangaliana usoni na kila mmoja atahakikisha anaangalia Kamera ili kupata picha inayowakilisha kujiamini mbele ya mwenzake.
- Rais akiwa anamsindikiza Rais mwenzake atahakikisha anakuwa wamwisho kuingia mlangoni, hii ni ishara ya Kiulinzi na kiusalama.
- Kuna Clip moja ya Video inayomuonyesha Mwenyekiti Yassier Arafat na Waziri Mkuu Ehud Barak. Clip hii inamuonyesha Ehud Barak akiwa wa mwisho kuingia kwenye chumba pale Camp David.
- Clip nyingine inayoonyesha Raisi George W Bush wa Marekani akimsukuma Waziri Gordon Brown kutangulia pale Number 10 Downing Street. Tendo hili liliwachukiza sana baadhi ya wanasiasa wa Uingereza (British political experts).
Ikumbukwe kuwa hadhi ya Kiraisi ni
MCHEZO (Game) kwakuwa sura iko mahali popote kidunia kwenye siasa. Sura ya Nchi inatafsiriwa zaidi kwa muonekano
wa Mtawala (Raisi) kwenye utawala wake. Raisi Barak Obama huwa anapenda sana
kuwashika Maraisi wenzake begani wakati wakusalimiana. Unaweza ukadhani kwamba
huwa analifanya kwa bahati mbaya na hakuwa amelipanga. Hebu jaribu kukumbuka jinsi
baba yako alivyokuwa akikushika bega ulipokuwa mtoto mzuri.
Inasemekana kuwa Raisi Bill Clinton alishindwa
kupata muitikio mzuri kwenye summit na Boris Yelsin wakiwa Moscow kwasababu Raisi
Clinton aliteguka Enka wakati anaingia Moscow. Hivyo ilibidi aingie na wheelchair
kwenye summit. Muonekano wa kigonjwa wa Raisi huyu wa Marekani wakati huo
ulipunguza umuhimu kwa wake kwa Boris Yelsin.
Inasemekana kuwa Ghana ilirejesha
heshima yake huko Afrika ya Magharibi wakati
Raisi Jerry J. Rawlings alipowasili kwenye Mkutano wa 25 wa OAU nchini Togo
Mwezi Julai 2000 akiwa kwenye Vazi la KIJESHI lililoonyesha Kujiamini kwa Raisi
huyu KIJESHI.
MUONEKANO WA RAISI NJE YA NCHI YAKE. RAISI ANAJIONYESHAJE??? RAISI ANAZUNGUMZAJE??
JE NI MUHIMU SANA????
Wakati Joyce Banda akichukua Madaraka
ya Uraisi ilionyesha wazi kama vile Malawi sasa itakuwa ikitekeleza yote
yatakayoelekezwa na Nchi jirani kwa dhana ya kuwa yeye ni Mwanamke. Kuna baadhi
ya magazeti ya Kiingereza walishangazwa sana na kutuita ‘a donor fearing
nation’.Raisi Joyce Banda alipoenda Landani
Uingereza alimuinamia Malkia Elizabeth wakati anamsalimia. Kitendo hiki
kiliwashangaza sana watu na Dunia Nzima kuwa kwanini alifanya hivyo wakati wote
ni viongozi wa Nchi??? Haya yote yameonyesha kuwa sura ya Utawala wa Malawi
niwakioga ulio na uwanajike ndani yake. Dunia ilianza Kusikia Mnuko wa Damu
kutokea Malawi baada ya Mwanamke kuingia madarakani. Sasa Tanzania imeamua na
kuona kuwa huu ndiyo wakati muafaka wa kuligawa Ziwa Malawi/Nyasi. Kumbuka kuwa
wazo hili halijawahi kuletwa wakati wa utawala wa Muluzi au Mutharika wakiwa Madarakani.
ZIWA MALAWI/NYASA |
Kama tukiruhusu wazo hili la Tanzania kudai ubainishaji wa Mipaka
sasa, kitakachofuata ni kudai pia na Chitipa? Msumbiji watadai Mlima wa Mulanje?
Serikali
ya Malawi lazima iweke wazi kuwa hakuna sehemu au eneo lolote nchini Malawi ambalo
litafanyiwa Majadiliano - full stop! Ni wakati wa Serikali ya Malawi kuonyesha
kujiamini. Waambie Tanzania kwamba Ziwa Malawi lilikuwa, ni na litaendelea kuwa
la Wamalawi.
Cha
kushangaza ni kwamba mbali na kauli mbalimbali za Tanzania Serikali yetu
haionyeshi reaction ya aina yoyote badala yake. Waziri wetu wa Mambo ya Nje wa
Malawi ametoa kauli kuwa suala hili litajadiliwa, Wewe Waziri?? Kwanini Hivyo??
Je unapanga kuwapatia Watanzania eneo ambalo si mali yao??? Je Unampango wa
kuligawa Ziwa?? Kwanini unaleta maamuzi ya kirafiki yasiyo na maslahi kwa
Wamalawi??? HAIWEZEKANI NA HATUTAKUBALI.
Huyo mwandishi ana agenda ya uchaguzi wa rais Malawi. Anajua kwamba Lazima Malawi iridhie ukweli kwamba Tanzania inamiliki sehemu ya mashariki ya ziwa Nyasa. Huyu mwandishi ni adui ya usawa wa kijinsia kwa kuandaa ajenda kuonyesha rais wao ni dhaifu kwa kuwa ni mwanamke. Mtu mbaya sana.
ReplyDeletePicha ya chini: Eti hao jamaa walioko beach wakitumbukiza mguu tu ndani ya maji wako Malawi. Hata hapo walipoketi wakati wa high tide ni Malawi,laah mpaka gani..
ReplyDelete