Napata kigugumizi juu ya hii dhana ya ukamataji wa Kazi FEKI za Wasanii. Nimesoma kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kuona juhudi kama si jitihada za Kampuni ya MSAMA PROMOTIONS ILIYOPEWA DHAMANA kama si kujipa DHAMANA ya kukamata kazi hizo feki za Wasanii. Swali langu ni kwamba umeshamkamata huyu mtengeneza kazi FEKI, tunaona kwenye vyombo vya habari kwa muda sasa vifaa mbalimbali vikiwa vimekamatwa kama picha zinavyojionyesha. Sasa mwanatanga ingependa pia kujua upande wa pili wa shilingi wa KINACHOENDELEA BAADA YA KUKAMATWA. Tunaona wakikamatwa lakini hatuoni wakichukuliwa hatua stahiki. Tunaomba sasa ufike wakati wa Jamii kuona upande wa pili wa shilingi kinachoendelea baada ya kukamata kazi hizo.
Isije ikawa tunakamata kazi hizi halafu tunazifungia majumbani mwetu au maofisini mwetu na baadaye kuzirudisha mitaani kwa mlango wa nyuma. Nashauri kama bidhaa hizi zimedhibitika kuwa ni FEKI hadi kuonyeshwa kwa Waandishi wa Habari basi zichomwe moto pia mbele ya Waandishi wa Habari na tuambiwe pia adhabu wanazopewa hao wahusika. Hongera kwa wale ambao mnafanya kazi hii lakini tunadhani ukamilifu wa zoezi hili nikuonyeshwa pia hatua mbele ya waandishi wa habari na si kuishia hapo.
Mungu awasimamie wale wote wenye nia njema katika zoezi hili la Ukamataji wa Kazi FEKI.
kurungezi
wa kampuni ya MSAMA PROMOTION, Bwa. Alex Msama pichani akifafanua jambo
kwa Wanahabari (hawapo pichani), kuhusiana na tukio zima la kamata
kamata ya wezi wa kazi za wasanii iliyofanyika mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment