BM BARBERSHOP KINONDONI

Thursday, August 9, 2012

YANGA MPIRA WA MAGAZETINI SIMBA MPIRA WA KWENYE MABANGO

BANGO LILILODHIHIRISHA KUWA MPIRA HUCHEZWA NA MABANGO
Bango hili lilinifanya nijirejeshe miaka kadhaa nyuma na kumkumbuka ndugu yangu Mwina Kaduguda alipokuwa Katibu wa FAT kwa kipindi ambacho nadhani hakikuzidi siku 90 alipotoa maamuzi ya kuipeleka timu ya Simba kwenye Mashindano ya Kimataifa KIMABAVU wakati hawakuwa wamefuzu kwa hatua hiyo na baadaye akawa Katibu wa Simba. Nikajirejesha pia kwa Mwenyekiti wa sasa wa Timu ya Simba na Mbunge wa Tabora Mjini Mheshimiwa Alhaji Ismail Aden Rage mwaka 1997  wakati Yanga ni Mshindi wa kwanza na timu ya Sigara mshindi wa pili na Simba mshindi wa tatu.. Kwa vigezo hivi Yanga ilipaswa kucheza Klabu Bingwa, Sigara Kombe la Washindi Barani Africa na Simba Kombe la CAF. Kituko kilikuwa ni pale Rage alipoamua kuipeleka timu ya Simba Kombe la Washindi na Sigara kuipeleka Kombe la la CAF ambalo sasa linaitwa kombe la Shirikisho.  

Najaribu kuona na kupima kidole kinachonyooshwa kwa bwana Angetile Osiah huku nikiwa na kumbukumbu kuwa Angetile huyuhuyu chini ya shinikizo la Rage aliipoka Yanga Point tatu dhidi ya Coastal Simba wakamsifia sana lakini leo inakuwa tofauti mpira wa bongo FULL MAJUNGU NA MIZENGWE.

TUKIO HUSIKA




Katika kukamilisha hafla kubwa ya siku ya Simba katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, klabu Simba imeshindwa kuwapa furaha mashabiki wake baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1 toka kwa timu ya Nairobi City Stars. Mchezo huo ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya kutangaza na kuwatambulisha wachezaji wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao wa kimashindano kwa klabu hiyo kongwe nchini. Simba iliwatambulisha wachezaji wake wote kama ifuatavyo;

1. Juma Kaseja Juma
2. Said Nassoro Collo
3. Haruna Moshi
4. 
5. Mbuyu Twite
6, Ramadhani Chombo Redondo
7. Uhuru Selemani
8. Kanu Myavangwa
9. Danny Mrwanda
10. Felix Sunzu
11. Abdallah Juma
12. Slim Kinje
13. Mussa Mude
14. Mwinyi Kazimoto
15. Shomary Kapombe
16. Mrisho Khalfani Ngassa
17. Amir Maftaha
18. Ahmed Waziri
19. Paulo Ngalema
20. 
21. Kiggi Makassy Kiggi
22. 
23. 
24. Juma Nyosso
25. Emmanuel Okwi
26. Haruna Shamte
27.
28. Amri Kiemba
29.
30.

Technical Bench
1. Milovan Circovick - Kocha Mkuu
2. James Kisaka - Kocha wa Magorikipa
3. Kessy Rajabu

Hata hivyo katika mchezo wa huo Simba haikuonyesha soka la kuwafurahisha mashabiki wake mbali ya kuonekana kocha Molovan Circkovic akibalisha wachezaji wake kila mara ambao waliufanya mchezo huo kudorora zaidi huku wapinzani wao Nairobi City Stars kuonekana wakifanya vizuri hususani katika kipindi cha pili ambapo walifanikiwa kuandika mabao yao yote matatu. Kimsingi kocha ana kazi ya kujua vema kikosi chake cha kwanza kwani bado wachezaji wa Simba hawajafahamiana vema hasa sehemu ya kiungo ambapo kuna Mwinyi Kazimoto,Haruna Moshi,Amri Kiemba,Kanu Mbiyavanga kila mmoja kuonekana ana uwezo binafsi. Hata hivyo ukiachana na mchezo huo kwa ujumla tamasha hilo limefana sana kwani mapema kulifanyika zoezi la kutoa misaada katika hospitali ya Mwananyamala, kisha michezo ya timu za wanawake katika uwanja wa Taifa ambapo ilitambulishwa timu ya Simba ya wanawake na hata tuzo mbalimbali kutolewa kwa wachezaji kama ifuatavyo:

Tuzo ya Nidhamu - Shomari Kapombe
Mchezaji Bora Msimu uliopita - Emmanuel Okwi
Tuzo ya Heshima - Marehemu Patrick Mafisango
Tuzo ya Heshima - Mzee Hamisi Kilomoni
Mchezaji Bora Miaka ya 1960 - Hamisi Kilomoni Ally Mchezaji Bora miaka ya 1970 -Haidari Abeid ‘Muchacho’ Tuzo ya Heshima ya Udhamini) – Mzee Ally Sykes Mchango wa muda mrefu klabuni - Profesa Philemon Sarungi  
Tuzo ya Mdhamini wa Sasa - Gaorge Kavishe, Meneja wa Kilimanjaro Beer.
 
Katika mechi ya kwanza, timu na wanawake ya Simba, Simba Queens iliifunga Ever Green ya Temeke mabao 5-3 katika mchezo wa Ligi ya Wanawake Shujaa wa Simba Queens alikuwa ni Maimuma Hamisi ‘Ronaldo’ aliyefunga mabao matatu.




No comments:

Post a Comment