HABARI
HII IMEANDALIWA NA BLOG YA BIN ZUBERY
MAKAMU MWENYEKITI WA SIMBA KABURU NYANGE AKITOA MAELEZO YA USAJILI WA MRISHO NGASSA PAMOJA NA MIKAKATI YA SIMBA MSIMU WA 2012/2013 |
KATIKA kile kinachoonekana kuwa
ni kutaka kuwakomoa mahasimu wao wa jadi, Yanga, klabu ya Simba imetangaza kuwa
tayari kumuuza straika wao Emmanuel Okwi kwa dau kufuru la dola za Marekani
milioni 2, ambazo ni sawa na Sh. bilioni 3. Bei hiyo ya Okwi kwa Yanga inazidi
mara 13 ya kiasi cha pesa walichokihitaji Simba wakati wakimuuza straika wao
Mbwana Samatta kwenda klabu tajiri ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo, ambayo ilikuwa ni dola za Marekani 150,000 tu, sawa na Sh. milioni 230! Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden
Rage, ndiye aliyetangaza dau hilo linaloonekana wazi kuwa na dhamira ya kufuta
ndoto za Yanga kumtwaa Okwi wakati akizungumza kwenye mkutano wa klabu hiyo ya
Msimbazi uliofanyika kwenye ukumbi wa Bwalo la Mafisa wa Polisi Oysterbay
jijini Dar es Salaam.
MAMIA YA WANACHAMA WA SIMBA WAKIWASILIKILIZA VIONGOZI WAO WAKATI WA MKUTANO |
Aidha, dau hilo la Okwi pia
linazidi takriban mara mbili ya bajeti ya Simba kwa mwaka ujao wa fedha ambayo
ilisomwa jana kwenye mkutano huo na kukadiriwa kuwa haitazidi Sh. bilioni 1.6.
Rage alisema kuwa Okwi bado ni
mchezaji halali wa klabu yao na kama Yanga wanamuhitaji kweli, basi watoe fedha
taslim kiasi cha dola za Marekani milioni 2 (Sh. bilioni 3).
WANASIMBA WAKIWA MKUTANONI |
Hata hivyo, inakumbukwa kwamba
ni wiki iliyopita tu, Simba ilisema kuwa inatarajia kumuuza Okwi kwa euro
600,000 (sawa na Sh. bilioni 1.1) kwa mabingwa wa Austria, klabu ya Redbull
Salzburg ambayo ilishiriki hivi karibuni ilitoka kushiriki hatua ya awali ya
Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Viwango tofauti vya bei ya
mchezaji huyo, vinamaanisha kwamba Simba iko tayari kumuuza Okwi kwa bei poa
Ulaya kuliko kumuona anajiunga na Yanga; na kwamba thamani ya straika huyo wa
kimataifa wa Uganda ni mara 13 ya Mbwana Samatta waliyemuuza kwa TP Mazembe.
Akieleza zaidi kwenye mkutano
huo uliohudhuriwa na wanachama zaidi ya 700, Rage alisema kuwa kwa vyovyote
vile, Okwi hawezi kukataa ofa ya mshahara wa euro 30,000 (sawa na Sh. milioni
57) kwa mwezi nchini Austria na kujiunga na watani zao, Yanga ambao
wanasemekana wako tayari kumlipa mshahara wa Sh. milioni 2.5 kwa mwezi endapo
atakubali kujiunga nao.
No comments:
Post a Comment