Hizi ni taarifa za awali za kuwajuza wapenzi wa blog hii walioko ndani na Nje ya nchi hii, taarifa kamili juu ya mpambano huu ambao umemalizika kwa Timu kufungana mabao 4-3 (Simba 4 na Mtibwa 3). Juhudi za kumpata Mchezaji wa zamani wa Mtibwa na Taifa Stars aliyekuwa amejijengea Heshima wakati anastaafu Soka ambaye sasa ni kocha wa Timu ya Mtibwa bwana Meck Mekisime zinaendelea na blog yako itakujuza kwa kina pamoja na Habari kwa njia ya picha baadaye.
Hatimaye kikosi cha pili cha mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Simba ya jijini kimefanikiwa kutwaa taji la michuano ya BankABC Sup8R 2012 baada ya kuichapa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa mabao 4-3 mchezo uliofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana mabao 3-3 huku mabao ya Simba yakiwa yamewekwa nyavuni na Christopher Edward mawili na Haroun Athumani na kwa upande wa Mtibwa mabao yao yakifungwa Shabani Kisiga mabao mawili na Hasan Seif.

No comments:
Post a Comment