Utaratibu wa bendi hapa nchini ulifuata sana
utaratibu wa bendi za nje kutokana na muziki wa bendi kuwa ni wa mapokeo. Hapa
naongelea aina ya vyombo vilivyotumika stejini. Katika rekodi za kwanza zaidi
za bendi kama vile zile za Cuban Marimba bendi zilipiga bila chombo chochote
kilichotumia umeme kwa kuiga staili ya Cuba, na pia teknolojiaa ya vifaa vya
umeme ilikuwa bado kuingia. Hivyo kulikuwa na gitaa moja na ngoma za kizungu
(drums), bongoz, na vyombo vya kupuliza, filimbi, trumpet, saxaphone. Nyimbo za
zamani za Salum Abdallah na Dar es Salaam Jazz Band zinatoa picha za vyombo
hivyo. Mwanzoni mwa miaka ya 60, vifaa vya umeme vilianza kutumika na bendi kwa
kawaida zilikuwa na Gitaa la bezi, rithim na solo,tarumbeta na saksafon. Halafu
kulikuwa na bongoz. Baadae tumba zilichukua nafasi ya bongoz. Baadae bendi
ziliingiza gitaa jingine ambalo liliitwa second solo. Hili lilikuwa gitaa
ambalo lilipigwa katikati ya rithm na solo. Cuban Marimba katika kipindi fulani
cha Mzee Kilaza aliweza kuongeza gitaa jingine waliloliita chord gitaa.
Kuingia kwa vinanda kuliliondoa gitaa la second solo katika bendi, japo kwenye bendi kama Tancut almasi na Vijana Jazz gitaa hilo liliendelea sambamba na kinanda. Kinanda pia kikachukua nafasi ya tarumbeta na saxaphone katika bendi nyingi. Kwa bendi zile ambazo zilikuwa zikifuata muziki wa magharibi mpangilio wao haukuwa na mfumo maalumu kutokana nani aina gani ya muziki wanafuatia. Mpaka sasa bendi kama The Kilimanjaro kwa kawaida hupiga gitaa moja,vinanda vitatu, gitaa la bezi, drums na conga au maarufu tumba. Wakati bendi kama Shada ni wana kinanda magitaa mawili na ngoma ya kiasili. Tatizo kubwa sana sasa ni bendi zinaigana katika mfumo katika kila kitu ubunifu ziro. Franko Makiadi aliondoka kwenye mfumo wa second solo akawa na solo gitaa 2, yeye mwenyewe akipiga solo na akawa na mpiga solo mwingine katika wimbo uleule. Ni wakati sasa wanamuziki kuangalia nyuma na kuona ni nini wanaweza kujifunza kitakachofanya muziki wao uwe tofauti na wa wengine.
No comments:
Post a Comment