GAZETI LA DAILY NEWS LA JUMATANO 22/05/1985
MAOFISA TISA WA NGAZI
YA JUU WA CDA WAFUKUZWA
Rais Nyerere amewafukuza wafanyakazi tisa wa CDA mara moja
na ameagiza marekebisho ya haraka yafanyike kwenye idara ili kuokoa mamlaka
hiyo.
Maagizo haya yametolewa jana na
Ikulu na kusainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Ofisi ya Rais Ndugu Timothy Apio.
Aliwataja maofisa hao waliofukuzwa kuwa ni pamoja na; Mkurugenzi
Mkuu Ndugu Joshua D. Minja, Mkurugenzi wa Makampuni ya CDA Ndugu Cecil J. Maruma
na Mkurugenzi wa Fedha Ndugu Jacob Mollel.
Wengine ni Katibu wa Ushirika
Ndugu Richard Rweyongeza, Mkurugenzi wa Ubunifu Ndugu William Feuzi, Kaimu
Maneja Ugawaji Ndugu Mathew Maselle, Kaimu Meneja Manunuzi Ismail Aden Rage,
Ofisa Mahusiano Ndugu Mavunde na Mkurugenzi wa Mipango Ndugu William Kitonka. Rais pia amemuagiza Waziri
anayehusika na Uendelezaji wa Mji wa Dodoma kufanya marekebisho kwenye Mamlaka
hiyo kama ifuatavyo;
·
Idara ya Fedha na Utawala iwe chini ya
Mkurugenzi wa Utawala aliyepo Ndugu A. Madata.
·
Idara ya Ubunifu na Ujenzi iwe kitengo cha
Ubunifu chini ya Ndugu R.K. Sigh wakati Idara ya Mipango itaendelea kuwa kama
ilivyo chini ya Ndugu Mpoli.
Watano kati ya maofisa hao waliofukuzwa akiwemo
Mkurugenzi Mkuu walipewa nafasi hizo mwezi Desemba mwaka 1983 baada ya
waliokuwepo kuondolewa kutokana na malalamiko kutoka kwa wananchi na wafanyakazi
wa CDA kuwa wanafuja mali. Mkurugenzi Mkuu Bwana Minja
alikuwa ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mijini.
Waliofukuzwa mwaka 1983 walikuwa
ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu Ndugu Moses Kagya, Mkurugenzi wa Makampuni ya CDA
Ndugu Kaboko Mutalemwa, Afisa Utawala Ndugu Philip Saiguran. Personal Oficcer
Ndugu F. Kamugisha. Kufukuzwa kwao kulitokana taarifa ya tume iliyoundwa Juni
1983 kuchunguza ubadhilivu ndani ya CDA chini ya Judge William Maina ambayo
ilibaini kuwa Maofisa wa CDA walikuwa wakijihusisha na uzembe, kuwasilisha
ripoti zisizo sahihi kwenye Bodi ya Wakurugenzi na utendaji usioridhisha.
Matumizi ya Mabaya ya magari ya CDA.
Mapema mwaka uliopita Rais
Nyerere aliunda tume iliyoongozwa na Waziri Mkuu ili kuharakisha uhamiaji wa
Mji Mkuu kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma. Maamuzi ya kuhamisha Makao Makuu
yalichukuliwa na Chama na Serikali Oktoba 1973 lakini mpango huo umekuwa
ukisuasua kutokana na utendaji mbovu wa viongozi wa CDA.
No comments:
Post a Comment